Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MWALIMU wa Ujasiriamali katika Chuo cha VETA- Karagwe mkoani Kagera Hamiss Jumanne amesema kwamba chuo chao kimekuja na ubunifu wa kutengeza Wine(Mvinyo) unatokana na tangawizi, Mchaichai na Amdalasini ambayo ni tofauti kabisa na aina nyingine za Wine zinazotengenezwa ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumza na Michuzi TV katika Banda la VETA lililopo kwenye Maonesho ya 46 ya  kimataifa ya Biashara yanayoendelea viwanja vya Sabasaba mkoani Dar es Salaam Mwalimu Jumanne amesema katika maonesho hayo yenye ujumbe unaosema Tanzania ni mahali sahihi kwa uwekezaji na masuala ya biashara wao VETA –Karagwe wameamua kuja na ubunifu wa kipee wa kutengeza Wine hiyo.

“Sisi VETA Karagwe tumekuja na kitu cha ubunifu kabisa na cha kipekee utengenezaji wa Wine kwa kutumia Mchaichai ,Amdalasini, Rozela pamoja na Tangazi ,huu ni utofauti mkubwa sana na ubunifu wa kipee ambao pia tumekuwa tukiwafundisha wanafunzi wetu kuona thamani ya vituo vingine.

“Wamezoea Mchaichai na Amdalasini unatumika kwenye chai tu lakini leo kwa ubunifu wetu uko kwenye Wine , ukiweka Wine kwa namna hii wanafunzi wakienda mtaani wataamua kujitegea wenyewe kwasababu watakuwa wamepata maarifa haya lakini itaongeza thamani na uchumi kwa wananchi.

“Ule Mchaichai na tangawizi vitalimwa kwa wingi sana ili waweze kuleta viwandani na viwandani vingine vinaweza kukua, kumbuka wanafunzi hawa ndio watakuwa wakurugenzi wa baadae.Kwa hiyo Wine hii ni tofauti na Wine nyingine kwani tuna fahamu zipo Wine zinazotengenezwa na Zabibu na Rozela lakini VETA Karagwe tumekua na Wine inayotokana na tangawizi, mchaichai na amdalasini.”

Amesisitiza hivyo Wine hiyo ni ya upekee kabisa unayoipata wilayani Karagwe Kagera na inafahamika kwa jina la Kombucha na mchanganyiko wake pamoja na mambo mengine umekuwa unasaidia kusafisha na kuimarisha mishipa, hivyo hata kwenye  suala la tendo la ndio linakuwa liko vizuri lakini hairuhusiwi kwa walio na umri chini ya miaka 18.

Amefafanua kwa anayetaka Wine hiyo kwa sasa wako Sabasaba na wanaohitaji wanakaribishwa banda la VETA.“Lakini unaweza kupiga simu 0759 817029 ina maana ukiwasiliana na sisii basi tunakuletea popote ulipo kwani Serikali yetu imerahisisha masuala ya usafiri.

“Sisi kutoka Karagwe basi ikitoka kule asubuhi saa nane usiku inakuwa imefika Dar es Salaam na Wine itakuwa imekufikia.Watu wanavutiwa sana kwani kila ambaye ananunua anarudi tena kutokana na ule uasili uliomo kwenye Wine yetu.”

Mwalimu wa Ujasiriamali katika Chuo cha VETA- Karagwe mkoani Kagera Hamiss Jumanne akiwa ameshika Wine ya Kombucha ambayo imebuniwa na chuo hicho baada ya kuchanganya Tangawizi, Mchaichai na Amdalasini .Wine hiyo imekuwa ni ya kibuni na ladha yake iko tofauti na ladha za wine nyingine.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...