Na Karama Kenyunko, michuzi Blog

CHUO Cha Taifa Cha Usafirishaji(NIT) kimewataka watanzania wenye malengo ya kufanya kazi katika miradi ya kimkakati inayoendelea nchini kujiunga na masomo chuoni hapo.

Pia kimesema kimefanikiwa kudahili wanafunzi wengi zaidi ya lengo walilojiwekea jambo linalowadhihirishia kukubalika kwao ndani na nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki na Ofisa Uhusiano Mkuu wa chuo hicho Tulizo Chusi wakati wa kuhitimishwa kwa maonyesho ya 17 ya Vyuo Vikuu yaliyoandaliwa na Time ya Vyuo Vikuu nchini(TCU) Jijini Dar es Salaam.

Amesema maonesho hayo yamewapa fursa watu wengi kufahamu undani wa masomo yanayofundishwa chuoni hapo.

"Tunazidi kuwasisitiza wale wote wenye malengo ya kufanya kazi katika miradi mbalimbali ya kimkakati inayoendelea hapa nchini na hata nje ya nchi kujiunga na NIT kwani tunaamini tunatoa elimu yenye ubora unaotakiwa," amesema Chusi.

Hata hivyo, amewapongeza TCU kwa kuandaa maonyesho hayo kwa kuwa mbali na kutoa fursa ya wanafunzi kufanya udahili wa moja kwa moja, yameviwezesha vyuo kujitangaza na hivyo kuwafanya wanafunzi kuelewa undani wa masomo wayapendayo.

Mkuu wa chuo cha NIT, Profesa Zacharia Mganilwa amesema ili kuongeza ufanisi na kusaidia sekta ya usafirishaji, chuo hicho kimeendelea kutoa mafunzo mbalimbali ya nadharia na vitendo kwa lengo la kutimiza adhma ya serikali.

Amesema NIT imeanzisha masomo yanayolenga kukidhi matakwa hayo na kuwataka wazazi na wananchi kwa ujumla kukitumia chuo hicho kikamilifu ili kufikia adhma hiyo hususani ya kuwaandaa wataalam wa kufanya kazi katika miradi mbalimbali ya kimkakati.

Manyesho hayo yalivishirikisha vyuo zaidi ya 75, yalianza Jumatatu iliyopita na kufunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, yalihitimishwa rasmi Jumamosi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Francis Michael kwa niaba ya Waziri Profesa Adolf Mkenda.

Akizungumza wakati akifunga maonyesho hayo, Michael amesema serikali itaendelea kufanya maboresho katika elimu ya vyuo vikuu nchini na mwaka huu zaidi ya mitaala 300 inafanyiwa mapitio ikihusishwa na maoni mbalimbali ya wadau.

Wananchi wakiendelea kumiminika kwenye banda la Chuo hicho cha NIT na kujifunza mambo mbali mbali yanayofanywa na Chuo hicho, wakati wa wiki ya maonesho ya 17 ya vyuo vikuu nchini, Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam yaliyokuwa yameandaliwa na Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU)


Mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Juma Mtanda akitoa maelezo kwa wanafunzi na wadau mbali mbali waliotemebelea banda Chuo hicho cha NIT na kujifunza mambo mbali mbali yanayofanywa na Chuo hicho, wakati wa wiki ya maonesho ya 17 ya vyuo vikuu nchini, Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam yaliyokuwa yameandaliwa na Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...