Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Techno Auditors, Lupiana Michael akizungumzia bonanza la michezo la timu za veterans ambazo zitachuana Jumapili (Julai 31) kwenye uwanja wa Bora Kijitonyama.


Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Techno Auditors, Lupiana Michael (kulia) akiangalia uwanja wa Kijitonyama (Bora) ambao utakaotumiwa na timu za saba za maveterans katika bonanza maalum lililopangwa kufanyika Jumapili (Julai 31, 2022). Pembeni ni mshauri wa masuala ya kodi wa taasisi ya Techno Auditors Richard Mabeba.


Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Techno Auditors, Lupiana Michael (kulia) akiwa katika majadiliano na katibu mkuu wa timuya Kijitonyama Veterans Amon Petro (Kiki) (katikati) na mshauri wa masuala ya kodi ya taasisi ya Techno Auditors, Richard Mabeba.

…………………………….

Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam

Jumla timu saba za maveterans zitashiriki katika bonanza maalum la mpira wa miguu litakalofanyika kesho Jumapili (Julai 31, 2022) kwenye uwanja wa Bora Kijitonyama.

Bonanza hilo limeandaliwa na taasisi ya ukaguzi wa mahesabu, ushauri wa kifedha, biashara na masuala ya kodi ya Techno Auditors kwa kushirikiana na timu ya Kijitonyama veterans.

Mkurugenzi mtendaji wa Techno Auditors, Lupiana Michael alisema kuwa mbali ya kuhamasisha maendeleo ya michezo, bonanza hilo litakuwa maalumu la kuadhimisha au kusheherekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwa taasisi yao.

Lupiana alizitaja timu hizo kuwa ni Tanga Veterans, Tabora Veterans, Goba Veterans, Uganda Veterans, Kijitonyama Veterans, Posta Veterans and Techno Auditors veterans.
Alisema kuwa bonanza hilo litaanza saa 2.00 asubuhi na timu zote zimetakiwa kuwahi kufika.
“Tumeweka masharti kwa timu zote shiriki ili kuwa na bonanza lenye mafanikio ya hali ya juu.Kwa mfano wachezaji vijana watakao ruhusiwa ni wanne (4). Kipa anaweza kuwa kijana pia na hatozuiliwa kucheza. Timu inaruhusiwa kuwa na vijana wengi, ila watakaoruhusiwa ni hao wanne tu.

Kanuni hiyo ina maanisha kuwa hata wakati wa ubadilishaji wa wachezaji lazima idadi ya vijana izingatiwe kwani akitoka kijana, ataingia kijana na haiwezekani atoke mzee aingie kijana. Lengo ni kuwapa nafasi wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 35 kupata muda wa kucheza,” alisema Lupiana.

Aifafanua kuwa kutakuwa na zawadi kwa mshindi wa kwanza na mshindi wa pili ambazo zitatolewa na waandaaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...