KATIBU wa siasa na uenezi wa mkoa wa Njombe Erasto Ngole,ametoa pongezi kwa wabunge na madiwani wa mkoa huo kwa kuwa mpaka sasa hakuna mbunge wala diwani aliyeitwa na Chama cha Mapinduzi ngazi ya mkoa kupewa onyo au kalipio kwasababu ya kukosa nidhamu kutokana na kutekeleza vizuri majukumu yao.

“Hakuna mpaka sasa diwani yeyote wala mbunge ambaje ameitwa na Chama cha Mapinduzi ngazi ya mkoa kwenda kupewa,onyo,adhabu au karipio kwasababu ya kukosa nidhamu na hii ni kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ya utekelezaji wa Ilani”Amesmea Erasto Ngole

Aidha Ngole amesema hali ya uchukuaji wa fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbali mbali ya uongozi ni ya kuridhisha kwa kuwa wagombea wamekuwa ni wengi ukilinganisha na mwaka 2017 hali inayoonyesha kukuwa kwa demokrasia ndani ya chama hicho

“Hali ya uchukuaji wa fomu kwa ajili ya uongozi kwenye nafasi mbali mbali inaridhisha kwa kuwa wagombea wamekuwa ni wengi ukilinganisha na mwaka 2017 na hii inaonyesha demokrasia ndani ya Chama chetu imeendelea kukua zaidi”aliongeza Ngole

Hata hivyo amebainisha kuwa hakuna kiongozi yeyote ndani ya Chama cha Mapinduzi mwenye hati miliki ya uongozi

“Hakuna mtu mwenye nafasi ya uongozi kwasababu nafasi zote ni za wana CCM,kwa hiyo kila mwanaccm anayosababu kushiriki kugombea lakini pia kupiga kura.Hata mimi ninarudi kwenye chujio ili wanaCCM wanipime kwa yale niliyoyafanya”Amesema Erasto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...