Wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, bachelor of science in Agriculture, Natural resources economics and business wakipata maelekezo kutoka kwa Ebeneza Mollel (Mwenye laptop) ambaye ni Mjiolojia kutoka PURA namna ya kujijisajili katika kanzidata ya watoa huduma wa kitanzania (Common qualification system).
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
WANAFUNZI wameshauriwa kutembelea panda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) ili kujionea fursa mbalimbali zinazopatikana katika taasisi hiyo kwa ajili ya kujiendelea na kupata ajira pindi watakapomaliza masomo hayo.
Ushaurii huo umetolewa jana na Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kitivo cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia ya vyakula ambao wanasoma kozi Uchumi wa kilimo, Maliasili na Biashara walipotembelea banda la PURA lililopo katika maonesho ya Biashara ya kimataifa ya 46 yanayoendelea Katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao, Katibu wa Chama cha Dar es Salaam University Agribusiness and Natural Resources Economic Association, Omary Mrisho amesema lengo la kutembelea banda hilo ni kujifunza uhalisi wa kile ambacho wamekuwa wakikisoma darasani katika maisha ya kawaida.
Amesema ziara yao imekuwa na matunda makubwa kwani wameweza kupata elimu kwa uhalisia na kugundua ndani ya PURA kuna fursa nyingi za ajira kutokana na mfumo wa mamlaka hiyo ya serikali.
Omary amesema PURA ni miongoni mwa taasisi za Serikali ambayo inafursa nyingi za kutoa ajira nyingi kutokana na kiwango cha elimu ya mtu, ikiwa pamoja na wenye ujuzi wa aina mbalimbali.
"PURA inafursa nyingi na kazi ambazo imekuwa ikizifanya ya utafutaji, uendelezaji kudhibiti na kubwa kinachohitajika ni mwamko mkubwa wa watu kuja katika maonesho haya katika banda la PURA kuja kujifunza kwani fursa zipo PURA," amesema.
Pia aliwashauri wanafunzi wengine kuwa na moyo wa kutaka kujifunza kitu badala ya kukaa darasani na kusubiri pekee watoke nje ili wapate fursa ya kujifunza zaidi kwa vitendo na uhalisia wenyewe.
Naye Mkuu wa kitengo cha ushirikishwaji wazawa na uhusishaji wadau kutoka PURA, Charles Nyangi amesema Mamlaka hiyo imepata Faraja na kunufaika katika maonesho hayo kwani watau mbali mbali wamepatiwa Elimu juu ya majukumu yake sambamba na kuwashirikisha fursa zinazopatikana PURA.
Mwanafunzi Omary Mrisho, wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kutoka kitivo cha Sayansi ya Kilimo na Teknolojia ya Vyakula (mwenye shati jeupe) akizungumza na waandishi wa habari kuelezea namna yeye na wenzake wanaosomea bachelor of science in Agriculture and Natural resources economics, walivyojifunza namna ya kujisajili katika kanzidata ya watoa huduma wa kitanzania (Common Qualification System) katika banda la Mamlaka ya Uthibiti Mkondo wa Juu wa Petrol (PURA) kulia kwake ni Mkuu wa kitengo cha ushirikishwaji wazawa na uhusishaji wadau kutoka PURA Charles Nyangi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...