
SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL,) limesema litaendelea kuboresha huduma
mbambali za shirika hilo ikiwemo kuongeza safari nyingi za nje ya nchi
ili kuweza kuendana na soko la kimataifa.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dar es salaam na Mkurugenzi ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi mara
baada ya kutembelea kampuni ya uwakala wa tiketi za ndege ya Skylink
Travel and Tours iliyopo jijini hapo.
Matindi amesema baada ya
kufanya vizuri kwenye soko la nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
kwa sasa wanajiandaa kwenda nchi za Afrika magharibi hapo mwakani baada
ya ujio wa ndege tano hivyo jambo lilopo sasa kwa ATCL ni kutatua
changamoto zinazoikabili.
Aidha,Matindi amesema kwa sasa
wamebaini kuna changamoto kwenye suala la tiketi ikiwemo abiria
kuchelewa kupata tiketi zinazochangiwa na kusuasua kwa baadhi ya kampuni
za ukataji tiketi na kuzitaka kampuni hizo kutatua changamoto hiyo kwa
kuwataka wateja kuweka umakini katika ukataji tiketi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa kampuni ya Skylink Travel, Moustafa Khataw amesema
wamemweleza Mhandisi. Matindi kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuzidisha vituo
vya Air Tanzania katika vituo vya kimataifa na wameafikiana kwamba
watakua wanakutana ili kuzungumza na kubadilishana mawazo kwaajili ya
Air Tanzania kwa ujumla.
Pia Khataw alihakikisha kuwa mawakala wa
Air Tanzania watashirikiana na Air Tanzania ili kupata muafaka mzuri wa
kupanua biashara kwa ujumla.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...