NA FARIDA SAID, MOROGORO.


Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Bwana.Mathayo Masele amelipongeza shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Morogoro kwa ubunifu waliofanya katika kuonesha teknolijia rafiki kwa wananchi hasa vijana wanaojiari ya kufunga umeme kwenye maeneo yao ya biashara.

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi alitoa pongezi hizo alipotembelea Banda la TANESCO kwenye maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki yanayoendelea mkoani Morogoro ambapo amewataka wananchi hususani vijana wanaosoma ufundi wa kufunga umeme kwenda kutembelea banda hilo ili kujifunza teknolojia hiyo.

“Kuna vijana wengi sana wanajiari kwenye biashara ya kuchaji simu za mkononi lakini ikienda pale unaona wanapata hasara kwa sababu mifumo ya umeme hawaijui wanafunga tu kutokana na ongezeko la wateja kwa hii ambayo naiona hapa itaweza kuwasaidia sana.” Alisema Mkuu wa Wilaya hiyo.

Kwa upande wake afisa uhusiano TANESCO Mkoa wa Morogoro Bi. Jacqueline Lusozi alisema mbali na teknolojia hiyo pia shirika lina mfumo mpya wa umeme tayaria (Umeta) ambao unampa fursa mwananchi wa kawaida kuweza kupata huduma ya nishati ya umeme bila ya kuweka mtandao wa nyaya( wiring) .

Umeta ni kifaa kidogo kinachotumika kusambaza umeme ndani ya jengo dogo la kuishi au biashara lenye chumba kimoja au viwili ambapo kinampa fursa mteja ya kuepuka gharama za kununua nyaya na vifaa vingine ikiwa ni pamoja na kumlipa mkandarasi gharama za kumfungia umeme.

Ukitumia umeta unaweza kufunga taa moja kubwa inayotosha kuangaza, swwichi kubwa itakayotumika kuwasha na kuzima umeme pamoja na kikata umeme( circuit breaker ) kwa ajili ya kuzima umeme ndani ya jingo inapotokea hitilafu .

Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Bwana.Mathayo Masele akiuliza maswali juu ya matumizi ya umeme tayari (umeta) alipotembelea banda la TANESCO kwenye maonesho ya nanenane kanda ya mashariki mkoni Morogoro wa kwanza kulia ni Kaim Meneja Tanesco Mkoa wa Morogoro Mhandisi Adam Abdallah.
.Afisa uhusiano TANESCO Mkoa wa Morogoro Bi. Jacqueline Lusozi akitoa maelezo ya matumizi ya umeta kwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Bwana. Mathayo Masele kwenye  maonesho ya nanenane Mkoani Morogoro.
Wakazi wa Mkoa wa Morogoro waliotembelea banda la TANESCO kupata elimu ya matumizi sahihi ya umeme.
 Maafisa wa Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro wakipata elimu kwenye banda la TANESCO kwenye maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki.

Afisa uhusiano TANESCO Mkoa wa Morogoro Bi. Jacqueline Lusozi akitoa maelezo kwa wananchi waliofika kwenye Banda la TANESCO kwenye maonesho ya nanenane kanda ya mashariki.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...