Na Mwandishi wetu, Dar
NAIBU Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Shirikisho la Ujerumani, Dkt. Bärbel Kofler amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku saba kuanzia tarehe 13 – 20 August 2022.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Dkt. Kofler amepokelewa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga.

Katika ziara yake nchini, Dkt. Kofler pamoja na mambo mengine, anatarajia kutembelea mradi wa ajira na ujuzi kwa maendeleo ya afrika (E4D) unaofadhiliwa na serikali ya Ujerumani, Kituo cha malezi na mafunzo kwa wasichana wadogo ambao ni wahanga wa biashara haramu ya binadamu kilichopo Kibamba na Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam.

Maeneo mengine atakayotembelea Naibu Waziri huyo ni pamoja na Kituo cha Afya cha Ngamiani na Hospitali ya Bombo mkoani Tanga, Zahanati ya Mkanyageni Wilayani Muheza, Halmashauri ya Jiji la Tanga, Asasi ya Tree of Hope iliyopo mkoani Tanga pamoja na Hospitali ya KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro.

Katika ziara yake nchini, Waziri Kofler anategemea kukutana na mawaziri wa sekta za afya, sheria, utalii, maendeleo ya jamii, fedha, nishati na maji kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Bärbel Kofler (katikati) akiongozana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga (kulia) baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa kutoka Ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Bärbel Kofler akisalimiana na Afisa kutoka Ubalozi wa Ujerumani nchini.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akimueleza jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani, Dkt. Bärbel Kofler walipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Shirikisho la Ujerumani Dkt. Bärbel Kofler akizungumza na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga walipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...