Kiongozi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba , Baba Halisi akitoa mahubiri wakati wa sherehe za kumleta Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake.



Waimbaji wa Kanisa Halisi la Mungu Baba wakiendelea kuiomba nyimbo za kumsitu na kumtukuza Mungu Baba wakati wa sherehe hizo.




Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MAELFU ya Waumini wa Kanisa Halisi la Mungu Baba kutoka ndani na nje ya Tanzania pamoja na waalikwa wa dini na madhehebu yote wamehudhuria Sherehe ya Kumletea Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake.

Sherehe hizo zimefanyika leo Agosti 28,2022 kwenye Kanisa Halisi la Mungu Baba lililopo Tegeta eneo la Namanga jijini Dar es Salaam ambapo pia Kanisa hilo limefanya maombi maalumu kuliombe Taifa pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan ili Mungu Baba aweze kumuungoza vema katika kulitumikia taifa

Kabla ya kuanza kwa sherehe ya kumletea Chanzo Halisi Matunda ya Shamba leke, Kiongozi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba Baba Halisi aliwaongoza wote waliohudhuria kufanya mambo kwa ajili ya Taifa la Tanzania ambalo limeendelea kubarikiwa kila uchwao.

Wakati maombi yakiendelea Baba Halisi alitumia muda mwingi kuongoza maombi kwa ajili ya Rais Samia Samia Suluhu Hassan ili Mungu Baba aweze kumlinda na kumpa afya njema ili aendelee kuwatumikia Watanzania.

Mbali ya kumuombea Rais Samia, pia waumini wa Kanisa hilo wakiongowa na Baba Halisi walifanya maombi kwa ajili ya kuombea mchakato wa Sensa ya Watu na Makazi ili iteelezwe kwa kiwango ambacho Serikali imekusudia hasa kwa kutambua sensa ni jambo muhimu kwa maendeleo ya wananchi wote.

Kuhusu Sherehe za Kumletea Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake , Baba Halisi ametumia sherehe hizo kuelezea kwa kirefu sababu za kuwa na kusanyiko hilo la kumletea Chanzo Halisi Matunda bila kujali dini au dhehebu.“Swali ni kwamba kwa nini sote tukusanyike kumletea matunda Chanzo Halisi bila kujali dini au dhehebu la yeyote?”.

Akitoa baadhi ya sababu amesema ni kutokuwa na tofauti ya behewa la nje na la ndani tena(Ufunuo 11:1-3).Waliotumwa walikuwa hawaruhusiwi kutoka nje ya kuta nne maana iliandikwa hivyo.

“Kwa kuwa yupo Chanzo Halisi mwenyewe ndani ya Moyo wa kila anayetenda haki (Isaya 57:15) yeye hazuiliwi kupima chochote.Maana katika Zekaria 14:9, yeye ni mmoja na jina lake ni moja,”amesema.

Ametaja sababu nyingine inayosababisha kumletea Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake bila kujali dini wala dhehebu ni kwamba ile barabara ya Mwafrika kuabudu Mwashukuru pamoja, tayari (Isaya 19:23-25).

“Iliandikwa kuwa itakuwepo barabara itokayo Afrika kwenda hadi Ashuru, yaani Uarabuni ambayo ni lugha safi(Sefania 3:10), hiyo barabara tayari ni lugha ya Kiswahili ambacho kimeenea kila mahali, hii ni sababu ya tatu ambayo imesbabisha sote tumletee Chanzo Halisi matunda ya shamba lake.”

Baba Halisi ametaja sababu nyingine ni Majira ya Simba na Ng’ombe kulisha pamoja(Isaya 11:7-9/Isaya 2:4).Majira ya Kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo wa Yohana , aliyekuwa anamiliki kila kitu ni Ibilisi kwa mujibu wa Luka 4:5-9.

“Sasa kila kitu kimerejea kwa Chanzo Halisi kwa mujibu wa Rumi 11:36.Illikuwa ni lazima tumletee Chanzo Halisi matunda ya shamba lake maana yeye anamiliki kila kitu kwa sasa na zaidi amewaponya mengi bila kujali dini wala dhehebu.

“Sababu nyingine ni kutokuwepo tena na njia mbaya za kupata utajiri.Wakati wa Majira saba ulikuwa huwezi kupata kitu kizuri mpaka utoe kafara kulingana na kitu unachokitafuta.

“Sasa kwa Chanzo Halisi hata kama uliua mke au mtoto ,Chanzo Halisi amekushika mkono ili yeye ndiye aonekane kwa kila kitu unachofanya.Usiogope tena kwa kujiuliza kuwa nitaanzaje kunyoosha wakati nilishakukosea , unapomtolea matunda leo, njia mbaya ya dunia ambayo ilikuwa na madai kwako haipo tena,”amesema.

Baada ya kutoa ufafanuzi huo Baba Halisi alitoa shukrani kwa waumini wa Kanisa Halisi la Mungu Baba pamoja na waalikwa wa madhehebu na dini zote ,amewashukuru wote kwa kujumuika kwenye sherehe hiyo ambayo yeye binafsi imemfanya awe mwenye furaha kubwa na anaamini hata wengine nao wamefurahi.

Pamoja na hayo Baba Halisi ameeleza kufurahishwa na wote ambao wamehudhuria sherehe hizo ambapo pia ametumia nafasi hiyo kutoa zawadi kwa makundi mbalimbali.

“Leo nimefurahi sana kwa wote mliohudhuria sherehe hizi za Kumeleta Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake bila kujali dini au dhehebu.”


Sehemu ya waumini na wageni waalikwa wakiwa wamesimama wakati wa ibada maalumu ya kuliombea Taifa pamoja na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa Sherehe za Kumletea Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake.

Mmoja ya Makuhani(kulia) akisoma neno wakati wa sherehe hizo.
Mmoja ya waumini wa Dini ya Kiislamu akitoa neno wakati Sherehe hizo baada ya kupewa nafasi ya kusalimia waumini wa Kanisa Halisi la Mungu Baba .


Matukio mbalimbali kwenye picha wakati wa Sherehe ya Kumletea Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake ambayo imefanyika leo Agosti 28, mwaka 2022 katika Kanisa Halisi la Mungu Baba lililopo Tegeta mkoani Dar es Salaam.


Kiongozi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba , Baba Halisi akitoa zawadi kwa mmoja ya mtoto wa waumini wa Kanisa hilo leo wakati wa Sherehe za Kumletea Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake.






Matukio mbalimbali kwenye picha wakati wa Sherehe ya Kumletea Chanzo Halisi Matunda ya Shamba lake ambayo imefanyika leo Agosti 28, mwaka 2022 katika Kanisa Halisi la Mungu Baba lililopo Tegeta mkoani Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...