Njombe
MAHAKAMA ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imemtia hatiani John Sevelini Chale (60) Mkazi wa Kijiji cha Iwela wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kwa kosa la kukutwa na hatia ya uchawi na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano (5) Jela.


Imeelezwa kuwa mnamo tarehe 01/02/2022 majira ya saa 08:30 asubuhi katika kijiji cha Iwela wilayani humo ziliripotiwa taarifa kuwa mshtakiwa anatuhumiwa kwa kujihusisha na vitendo vya kishirikina kutoka kwa mlalamikaji Hekima Antony Chale ambaye ni kaka wa mhanga Vediana Antony Chale ambaye ni mtoto wa mdogoake mtuhumiwa aliyeugua kichakaa kutokana na vitendo vya mshtakiwa

Mahakamani imeeleza kuwa baada ya upelelezi kukamilika mtuhumiwa alifikishwa katika Mahakana hiyo tarehe 01/03/2022 ambapo alisomewa shitaka moja la kujihusisha na vitendo vya kishirikina kinyume na kifungu cha 3(a) na 5(1) cha sheria ya uchawi sura ya 18 marejeo 2019 na mwendesha mashtaka wa serikali Asifiwe Asajile mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Ludewa Isaac Ayeng'o.

Mwendesha mashtaka wa serikali aliiomba Mahakama kumpatia mshitakiwa adhabu kali ili iwe fundisho kwake na jamii kwa ujumla kwani vitendo vya kishirikina vinasababisha migogoro ya familia na jamii kwa ujumla na kupelekea mauaji na baada ya hoja hizo Mahakama imeamuru mshitakiwa kutumikia kifungo cha Miaka 5 gerezani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...