Benki ya NMB leo imezindua rasmi
mashine ya kubadilisha fedha (Forex – ATM) katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) yenye uwezo wa kubadili fedha za kigeni
kwenda shilingi za Kitanzania. Hii ni hatua nyingine muhimu kwa Benki ya
NMB ya utoaji huduma kwa Watanzania wanaosafiri kutoka nje, watalii na
wageni wanaokuja nchini Tanzania.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzi uwanjani hapo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna
alisema, wateja na hata wasio wateja wa NMB sasa wanaweza kubadilisha
fedha hadi kiasi cha Dola za Kimarekani 2,000 kwa wakati mmoja kwa
viwango vya kubadilishia fedha vya Benki ya NMB kwa kujihudumia wenyewe
kwa kutumia mashine hii ya ATM katika uwanja huo. Aliongeza kuwa,
mashine hii pia inauwezo wa kubadilisha Euro za Umoja wa Ulaya na Pauni
ya Uingereza kwenda shilingi ya Tanzania.
Uzinduzi huu ni
muendelezo wa huduma hizo zilizozinduliwa kwa mara ya kwanza na NMB
Jijini Dar es Salaam kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere na Benki hiyo inatarajia kupeleka huduma hizo maeneo mengine
ikiwemo uwanja wa ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume (AAKIA) Zanzibar
na Zanzibar Stone Town.
Bi. Ruth alisizitiza kuwa, sasa watakao
hitaji kubadili fedha uwanjani hapo, watajihudumia wenyewe wakati wote
masaa 24/7 na wameanza na aina hizo tatu za sarafu, lakini muda sio
mrefu wataongeza na fedha za mataifa mengine.
Mgeni rasmi katika
hafla ya uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Kiliamanjaro Mhe. Nurdin Hassan
Babu aliipongeza Benki ya NMB kwa kuanzisha huduma hiyo muhimu kwani
imesubiriwa kwa muda mrefu mkoani hapo, ikizingatiwa kuwa mkoa huo
umekuwa ukipokea wageni wengi wa kigeni ambao ndio wenye uhitaji mkubwa
wa kubadili fedha.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Bi. Christina Makatobe, alisema
huduma hiyo ni muhimu kwa taasisi hiyo haswa ikitiliwa maanani KIA ni
lango la kuingilia wasafiri kwa wingi, wengi wao wakiwa ni watalii na
sasa hata wanaoingia uwanjani hapo nyakati za usiku watabadilisha fedha
kwa kujihudumia wenyewe – hii itakuwa kivutio cha watalii wengi nchini
kutokana na ukweli huduma bora haswa za kifedha ni moja ya vigezo
ambavyo watalii hufuatilia kabla ya kutembelea nchi husika.
Bi.Christina
aliiahidi kuendelea kushirikiana na NMB kuhakikisha wanaungana katika
kuweka mazingira mazuri ya kuboresha sekta ya utalii nchini hasaa
kupitia watumiaji wa uwanja wa KIA.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Hassan Babu akionyesha fedha za
kitanzania baada ya kubadili fedha za kigeni kwenye FX ATM ya NMB
iliyozinduliwa rasmi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA). Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth
Zaipuna(kushoto) na Mkurugenzi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro - Christine Mwakatobe.Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Hassan Babu akikata utepe kuashiria
kuizindua rasmi mashine ya kubadilishia fedha za kigeni kwenda Shilingi
za Kitanzania (FX ATM) ya NMB katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA). Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth
Zaipuna, Mkurugenzi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro -
Christine Mwakatobe na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ndg. Juma Irango
wakishuhudia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...