MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Godwin Gondwe ameipongeza kampuni ya Simu ya Vodacom kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kuleta mabadiliko yanayoigusa jamii moja kwa moja.
Gondwe ameyasema hayo leo, Agosti 29,2022 alipotembelewa na washindi wa bajaji na pikipiki kupitia kampeni ya ‘M Pesa imeitika’, .
Mheshimiwa Gondwe ametanabaisha kwamba Vodacom wamekuwa vinara katika mapinduzi ya teknolojia na huduma zinazonufaisha Watanzania wote.
“Vodacom walikua wa kwanza kufanya M PESA; Vodacom ilikua ya kwanza kuleta M-PAWA, Vodacom imeweza kuwa ya kwanza kuleta M-MAMA ambayo inasaidia kina mama kuweza kufika hospitalini haraka na wakapata huduma, ni jambo kubwa sana...., lakini pia Vodacom walikua wa kwanza kuleta 4G, kwa hiyo sisi kama Serikali tunawapongeza sana” amesema Gondwe.
Gondwe ameongeza kuwa, kupitia ‘M Pesa Imeitika’ na huduma nyingine za Vodacom, vijana wanafikiwa na kuweza kutengeneza ajira akitolea mfano kwamba bajaji na pikipiki zilizotolewa zitatoa ajira kwa vijana.
Nao washindi wa zawadi za bajaji na pikipiki kupitia kampeni ya M-Pesa Imeitika, Magdalena Magoma na Beata Madachi, wameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi yanayoziwezesha sekta binafsi na kampuni kama Vodacom kuweza kuchangia maendeleo ya vijana kama wao na jamii kwa ujumla.
Kampuni ya Vodacom inaendelea kuwa kinara kwa kuwa ya kwanza katika mapinduzi ya kidigitali na kuwa na huduma zenye ubora na kugusa maisha ya Watanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe (katikati) akiwa katika picha na washindi wa zawadi za bajaji na pikipiki kupitia kampeni ya M-Pesa Imeitika inayoendeshwa na Kampuni ya simu ya mkononi Vodacom, Magdalena Magoma na Beata Madachi, walipomtembelea ofisini kwake, leo Agosti 29, 2022 Mkoani Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...