Na Mwandishi wetu, Mirerani


Timu nane za soka zinachuana kwenye michuano ya Sensa Cup Bonanza inayotimua vumbi kwenye viwanja vya Tanzanite Complex Stadium, Mji mdogo wa Mirerani.

Afisa Tarafa ya Moipo, Joseph Mtataiko, akizindua michuano hiyo asubuhi ya Agosti 22 amesema Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Dkt Suleiman Hassan Serera, atahitimisha michuano hiyo jioni kwa kugawa zawadi mbalimbali kwa washindi.

Mtataiko amesema bonanza hilo lenye kauli mbiu ya "Wana Simanjiro tupo yatari kuhesabiwa" lina lengo la kuhamasisha jamii ya eneo hilo kushiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23.

"Serikali imetangaza kuwa siku ya sensa Agosti 23 itakuwa mapumziko hivyo wananchi wote watulie majumbani mwao na wahakikishe wanatoa ushirikiano kwa makarani wa sensa ili wahesabiwe," amesema Mtataiko.

Mwenyekiti wa chama cha soka Wilaya ya Simanjiro, Charles Mnyalu ametaja timu zitakazoshiriki Sensa Cup Bonanza ni Tanzanite Sports Academy, Green Light na Watumishi FC.

Ametaja timu nyingine ni Tanzanite Sports, Naisinyai SC, Charity FC ya Mbuguni Wilayani Arumeru mkoani Arusha.

"Pia kuna timu mbili za wasichana za Tanzanite Queens ya Mirerani na Tiger Queens ya jijini Arusha, ambazo nazo zitapambana," amesema Mnyalu.

Ametaja zawadi zitakazotolewa na DC wa Simanjiro kwenye Sensa Cup Bonanza ni kombe na mpira kwa mshindi wa kwanza, mipira miwili kwa mshindi wa pili na mpira mmoja kwa mshindi wa tatu.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...