Mtama, Lindi
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewahimiza Watanzania wajitokeze kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi, kwani zoezi hilo ni muhimu katika upangaji wa maendeleo ya nchi.


Aidha amesema takwimu zinaonesha mpaka sasa asilimia 98 ya Watanzania wanafahamu kuhusu zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika Agosti 23, mwaka huu.


Kauli hiyo ya Waziri Mkuu imetolewa leo kwa niaba yake na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye katika tamasha la UHURU FM SENSA MARATHON lililofanyika kwenye uwanja wa Majengo, Mtama, mkoani Lindi.


Amesema huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo afya,elimu na huduma nyingine, zitaboreshwa zaidi iwapo serikali itakua na takwimu sahihi za wananchi wake.


Akizungumzia watu wenye mahitaji maalumu,amesema watu hao ni lazima wahesabiwe ili nao takwimu zao zipatikane, na wahudumiwe vizuri na serikali.


Naye Mbunge wa Mchinga Mhe. Salma Kikwete amesema wabunge wa mkoa huo na wananchi wao,wamejipanga kuhesabiwa ktk zoezi la sensa ya watu na makazi.


Mama Kikwete amesema zoezi Hilo mwaka huu litafanyika kisasa zaidi, tofauti na miaka iliyopita.


Awali Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Uhuru Fm Bi. Amina Aziz, amesema kituo hicho cha redio kimeamua kuandaa marathon hiyo, kwa nia ya kuunga mkono juhudi za serikali ktk zoezi la sensa ya watu na makazi.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...