WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amewataka washiriki wa Mafunzo yanayohusu Manunuzi ya Umma kuhakikisha kuwa Mafunzo hayo yanawajengea Weledi na kuwawezesha kutekeleza Shughuli za manunuzi ya Umma kwa Uaminifu na Uadirifu.

Mheshimiwa Waziri ameyasema hayo katika Ukumbi wa JKT Chamwino alipokuwa akifungua Mafunzo ya siku mbili yanayohusisha Afisa Masuuli, Idara na Virengo tumizi, bodi za zabuni na Kamati ya ukaguzi ambapo pamoja na mambo mengine mheshimiwa Waziri kasisitiza kuwa Mafunzo haya ni muhimu sana iwapo mhusika hayupo tutakuwa tunapoteza fursa muhimu saana.

Waziri amesema Sekta ya manunuzi ni sekta muhimu sana katika Wizara na Taasisi mbalimbali, ufanisi katika manunuzi ya umma ni mhimiri katika ufanisi wa taasisi kwani kila mwaka Serikali hutenga fedha nyingi kwa ajili ya manunuzi, wakati wote ni matumaini ya Serikali kuwa fedha hizo zitatumika katika malengo yaliyokusudiwa na manunuzi yaliyozingatia taratibu, ubora na thamani ya fedha.

Waziri pia amewakumbusha washiriki wa mafunzo haya kuyatumia vizuri kwa kutanguliza maslahi mapana kwa nchi pindi wanapotekeleza majukumu yao ya msingi.

Aidha, Mheshimiwa Waziri amesema Mafunzo haya yanayotolewa na Wawezeshaji kutoka Mamlaka ya udhibiti wa Manunuzi ya Umma – PPRA yana lengo la kuwajengea uwezo taasisi za manunuzi ya Umma ambazo kwa mijubu wa sharia ya mwaka 2011 ikafanyiwa marekebisho mwaka 2016 na kurekebishwa tena mwaka 2022 zimepewa mamlaka tangu kuandaa bajeti na kuanzisha mahitajio hadi kukamilisha kwa manunuzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...