Na Mwandishi Wetu,Ludewa

MKAZI wa Kijiji cha Lusala wilayani Ludewa mkoani Njombe  Razalius Kufabasi (50) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumpigia na tofali la kuchoma Linus Mtega(52) na kumsababisha umauti.

Imeelezwa kwamba siku ya tukio hilo kulikuwa na shughuli ya kujengea makabuli ambapo usiku watu walikuwa wakiburudika kwa muziki, hivyo Mtega(sasa marehemu) huyo alikuwa amemkumbatia mke wa mzee Kufabasi huku wakicheza pamoja.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Michuzi TV na Michuzi Blog kwamba hali  hiyo ilisababisha mzee huyo wivu hivyo akaamua  kuchukua tofali na kumpiga nalo mzee Mtega kwenye paji la uso.

Akithibisha kutokea kwa tukio hilo kwa waandishi wa habari,  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema mzee Mtega alichanika kwenye paji lake la uso na kulazimika kukimbizwa kituo cha afya cha Mlangali lakini hakuweza kupona baada ya kufikwa na umauti.

Kamanda Issa amesema  mtuhumiwa baada ya kuona amesababisha kifo cha mzee huyo  akijaribu kutoroka lakini hakuweza kufanikiwa kwani Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumtia nguvuni ili sheria ichukue mkondo wake.

Aidha Kamanda Issa amelaani vikali tabia hizo huku akiitaka jamii kuacha wivu uliopitiliza kwani yanapotokea mauaji kama haya familia pamoja na watoto ndio huteseka.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...