AFYA ya Uzazi kwa Vijana ni msingi kwa kundi hili kujichanua na kufikia kiwango cha juu cha ndoto zao kwa kuwa moja kati ya Malengo ya melenia ili kuwa ni kuhakikisha huduma za afya ya uzazi kwa vijana zinaboreshwa ili kuendelea kuchangia maendeleo ya nchi.
Ni ukweli usiopingika kwamba wapo baadhi vijana wakikena wakiume bado hawana elimu ya kutosha juu ya ufahamu wa afya ya uzazi na uzazi wa mpango na kijana ili ajitambue anapaswa kuelewa mabadiliko yanayojitokeza katika mwili wake na kujua namna ya kudhibiti.
Elimu ya afya ya Uzazi kwa vijana itawapatia maarifa ya kujitambua,kufahamu mabadiliko yanaweza kuwatokea pindi wanapoendelea kuku ana namna ya kufanya maamuzi sahihi,kwa kuwa hali ya kukosa elimu sahihi ya uzazi imekuwa ikileta madhara hasa katika kujiingiza katika maambukizi ya magonjwa ya ngono ikiwemo,Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi,Mimba za utotoni pamoja na magonjwa mengine.
Wapo vijana ambao wamekuwa wakipata mimba katika umri mdogo,wapo wengine wamekuwa wakizaa watoto pasipo kufata suala la uzazi wa mpango na kupelekea ndoto zao kuishia njiani.
Zipo jitihada za Serikali pamoja na Mashirika mbalimbali ambayo yamekuwa yakitoa elimu nchini kuhusu umuhimu wa afya ya uzazi kwa vijana wakike na wakiume lakini bado kuna mtazamo hasi kuwa utoaji wa elimu hiyo ni kumfundisha mtu kufanya ngona jambo ambalo siyo kweli.
Pia,tunafahamu kuwa zipo baadhi ya Halmashauri na manispaa na zimeanza kupunguza maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na maradhi mengine ya zinaa,baada ya vijana wengi kuhamasika na kuhudhuria kliniki ya huduma rafiki kwa vijana zihusuzo afya ya uzazi na mtoto.
Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka 2030 kwa wa nachama wa Umoja wa
Mataifa ikiwamo Tanzania inatambua kuwa huduma ya uzazi wa mpango ni haki ya
kila mtu binafsi na mume na mke bila kujali mahali au namna wanavyoishi, au wana
pato la kiasi gani.
Sote tunafamu kwamba Tanzania suala la utoaji mimba hailiruhusiwi kisheria,pamoja na serikali kupitia Wizara ya Afya kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo utoaji wa mwongozo baada ya mimba kuharibika hivyo elimu inapaswa kuendelea kutolewa kwa kundi hilo la vijana.
Ikumbukwe kwamba,Tanzania ili Saini Mkataba wa Maputo ambayo ibara ya 14 2(c)inaeleza haki ya utoaji mimba lakini kwa kuzingatia sababu kadhaa ikiwemo kubaka au kufanya ngono na mtu wa karibu,lakini Tanzania bado kuna mtazamo wa kigezo kimoja za kutoa mimba jambo ambalo linahatarisha afya ya Mama.
Lakini pia,katika maazimio ya kikanda na kimataifa Umoja wa Afrika Mpango Endelevu wa Utekelezaji wa Maputo kuhusu Afya na Haki za Uzazi na Kijinsia 2016-2030,uliorejewa na Kifungu cha 14 (g) katika Itifaki ya Maputo juu ya Haki za Wanawake, ulitoa kipaumbele katika uwekezaji wa kitaifa ili kuhakikisha huduma za uzazi zinawafikia wote ikiwa ni pamoja na matumizi ya njia za kisasa za kuzuia mimba.
Vinaja wanauelewa wa kutosha kuhusu elimu ya afya ya uzazi.
Suzana Sumalu,mkazi mkazi wa Jiji la Dodoma anasema yeye mwanaume wake anapenda wazae watoto lakini hapendi atumie aina yoyote ya uzazi wa mpango.
“Mimi sasa hivi nina watoto wawili na wamepishana mwaka mmoja mmoja kuna haja ya watoa elimu ya afya ya uzazi wa mpango kutoa elimu hiyo hadi huku vijijini wasikae mijini pekee”,anasema Suzana
Wakati mwingine namwambia Mume wangu kuhusu kuhudhuria hata katika kliniki yeye anasema yuko bize kutafuta hela ila nitaendelea kumwelewesha kuhusu elimu ya uzazi .
Raphael idfonce,Mkazi wa Dar es Salaam Wilaya ya IlalaBaba wa mtoto mmoja anasema hajawahi kusikia elimu ya uzazi wa mpango na hawajawahi kufundishwa ila mke wake anaufahamu wa masuala hayo.
“Sijawahi kumwona mtu akija kunielimisha kuhusu umuhimu wa elimu ya uzazi wa mpango na tunaishi kwa kudra za Mwenyenzi Mungu”,anasema Idfonce
Idfonce anaishauri Serikali kutoa elimu ya afya ya uzazi kupitia vipindi mbalimbali kwenye redio au Runinga ili watu waendelea kupata hiyo elimu kwa sababu wengine huuenda wanaona aibu kushiriki.
Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Ilala Joyce Maketa anasema licha ya Serikali kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa afya ya uzazi kuna haja ya kuwepo kwa vitengo maalumu mashuleni au Vyuoni vya kutoa elimu ya afya uzazi.
“Elimu bado inahitajika kwa mfumo uliopo kwamba ni wakati gani kijana anapata elimu kuhusiana na afya ya uzazi,ukiwa kijana lazima kuwepo na mabadiliko sasa lazima waambiwe ukweli kwamba jambo hili madhara yake haya na haya,”anasema Joyce.
Anasema Mzazi inakuwa ni vigumu kumwambia mtoto wake moja kwamoja lakini watoa huduma ya maelezi au mahusiano kwa vijana wanaweza kumwambia mtoto wake,na wasipo fundishwa mwisho wake wanajikuta wanaingia katika mitandao kupata taarifa ili hali taarifa hizo pengine hazijachujwa kimaadili ya Kitanzania.
Joyce,kuwepo na majukwaa ya mara kwa mara yatakayofundisha masuala ya afya ya uzazi na Serikali iyatambue kabisa majukwaa hayo ili ijue elimu inayotolewa sehemu hiyo je inazingatia rika kwa sababu huende sehemu hiyo ikawa na watoto wadogo ambao hawastaili kusikiliza elimu hiyo.
Mara nyingi,naona mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yamekuwa yakijitahidi kutoa elimu hiyo hiyo lakini lazima nguvu iongeze ili kuepusha madhara mengine ambayopengine yangeweza kuzuilika mapema kwa vijana hao na kutimiza malengo yao.
Tutambue kuwa kazi ya utoaji elimu ya afya ya uzazi inaendeshwa kwa kuzingatia usiri mkubwa baina ya mtoa ushauri na mpokeaji majibu, hutolewa kwa muhusika tu bila kushirikisha mtu mwingine, hivyo kijana akielimika itamsaidia kuwa muwazi juu ya afya yake.
Lakini kila jambo linachangamoto zake, wakati ninaposema Serikali na wadau juhudi zao zinaonekana, lakini bado wakumbuke hususan Serikali kuwa bado kuna upungufu wa wataalamu wa kutosha wa kutoa elimu kwa vijana wa uelimishaji rika, muda wa watoa huduma kuwa mdogo na wataalamu kuwa na muda finyu kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine.
Halmashauri na manispaa nazo, zisichoke bali ziendelee kuchochea kwa kuhimiza elimu hiyo itolewee kwenye shule na vituo vya afya.
Kwasababu, kadiri vijana wanavyoelimika ndivyo wanavyoweza kujikinga dhidi ya maradhi ya zinaa, mimba za utotoni na kujitunza ili wawe na afya njema kukosa elimu ya uzazi kwa kundi hilo ni sawa kuwaweka hatarini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...