Na Fredy Mgunda, Iringa.
Wanyama pori wa Hifadhi ya Taifa Ruaha iliyopo mkoani Iringa wapo hatarini kutoweka kutokana na kuongeza kwa ujangiri unaodhofisha Ustawi wa wanyama hao ambo wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa kupitia utalii Hivyo maafisa tarafa na watendaji wa kata wametakiwa kutoa elimu ili kukomesha ujangiri huo.
Akizungumza wakati wa ziara ya Utalii ya maafisa tarafa na watendaji kutoka wilaya ya Iringa iliyoratibiwa na mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo,Kamishna msaidizi wa uhifadhi na Mkuu wa hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Meng`ataki alisema kuwa Kuna baadhi ya wananchi kwa makusudi wamekuwa na nia ovu ya kumaliza rasilimali ya wanyama kwa kufanya shughuli za ujangiri jambo ambalo halikubariki kwa jamii.
Meng'ataki alisema kuwa kijiji cha Tungamalenga kilichopo tarafa ya Idodi Wilayani Iringa kimetajwa kuwa kinara katika matukio ya Ujangari wa wanyamapori katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa kuhusika na matukio 79 kwa kipindi cha mwaka 2012-2022.
Meng`ataki alisema hali ya ujangili inazidi kuongezeka kutokana na wananchi kuwaficha wahalifu jambo linalohatarisha usalama wa wanyamaa
Alisema kuwa agenda ya kupinga ujangili iwe kipaumbele kila wakati kwenye vikao vya serikali ambavyo sio vya kiserikali kwa lengo la kuendelea kutoa elimu ya kupinga ujangiri ambao unafanywa na wananchi wanaoizungu hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa kiasi kikubwa ili waache tabia hiyo.
Meng'ataki alisema kwa sasa hali inazidi kuwa mbaya inayowakabili wanyamapori katika hifadhi ya taifa ya Ruaha mkoani Iringa kutokana na kuongezeka kwa ujangiri.
Kijiji cha Kalenga kilicho jirani na hifadhi hii ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini ndiyo kinatajwa kinara, katika matukio ya ujangiri unaozohofisha ustawi wa wanyama na rasirimali hii muhimu inayochangia pakubwa katika pato la taifa kupitia utalii
"Nitolee mfano jana tu katika Kijiji cha Ismani tumekamata Bunduki mbili,risasi kadhaa,mafuta ya simba,pua za nguruwe na vitu vingine kwa hiyo watu wanakuja kumaliza wanyama pori huku wakati viongozi wa Vijiji,kata na tarafa mpo"alisema Meng'ataki
Meng'ataki alisema kuwa wanyama pori wapo hatarini zaidi kutokana na kukosekana kwa uzalendo wa wananchi kuilinda rasirimali hiyo kwa kuwafichua majangiri ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa
Kamanda huyo wa Uhifadhi alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika ulinzi wa Wanayama pori katika hifadhi hiyo na nyinginezo nchini
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho alisema kuwa kulinga na umuhimu wa hifadhi hiyo kwa taifa ni vyema kila mmoja akawa balozi wa kupinga ujangiri kwa kutangaza na kushuiriki katika vita ya kutokomeza uhalifu huo
Moyo alisema kuwa uhusiano utakaoimarishwa baida ya viongozi wa serikali za vijiji kata na Tarafa hasa za jirani na maeneo yote ya hifadhi utasaidia pakubwa kampeni hiyo hiyo maalum katika kutokomeza ujangili.
Nao baadhi ya watendaji wa kata walisema kuwa wataenda kutoa elimu ya umuhimu wa uhifadhi wa wanyama pori na faida zao kwa jamii ili kuhakikisha wanaondoka na shughuli za ujangiri na kuukomesha kabisa kwa maslai ya Taifa.
Kamishna
msaidizi wa uhifadhi na Mkuu wa hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell
Meng`ataki akiongea na watendaji wa kata pamoja na maafisa Tarafa juu
ya umuhimu wa kutoa elimu ya uhifadhi wa wanyama pori na kukumesha
vitendo vya ujangiri katika hifadhi hiyo
Mkuu
wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa na baadhi ya maafisa
Tarafa na watendaji wa kata wa wilaya ya Iringa wakati wa ziara ya
utalii katika hifadhi ya Taifa ya RuahaKamishna
msaidizi wa uhifadhi na Mkuu wa hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell
Meng`ataki na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo wakiwa kwenye
picha ya pamoja na maafisa Tarafa na watendaji wa kata wa wilaya ya
Iringa wakati wa ziara ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha kwa lengo
la kuongeza utalii wa ndani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...