Na Mwandishi Wetu, Geita
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Geita kwa ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu uliojengwa kwa kushirikiana na Mgodi wa Madini ya Adhabu wa Geita (GGM).
Aidha, Kinana ametumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wa mkoa huo pamoja na GGM kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa uwanja huo haraka ili kuanzia sasa hadi inapofika mwaka 2027 uwe umekidhi vigezo vinavyotakiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Kinana ameyasema hayo leo Septamba 4,2022 baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa uwanja wa Magogo unaojengwa ndani ya Halmashauri ya Geita ambao ujenzi wake kwa awamu ya kwanza unaendelea kwa kasi kubwa, lakini ameomba waukamilishe.
"Niwapongeze GGM kwa ujenzi wa uwanja huu mzuri na wa kisasa, wamejitahidi kuumaliza uwanja huu kwa wakati kwa sababu ni uwanja muhimu kwa Mkoa wa Geita. Niwaarifu nadhani wiki mbili au moja iliyopita, kulikuwa na mkutano wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) jijini Arusha.
"Lakini sio hivyo tu, Rais Samia Suluhu Hassan anadhamira ya kuleta mashindano ya Kombe la Afrika mwaka 2027 nchini Tanzania, ndugu zangu wa Geita nimewasikia mkisema lengo lenu ni kuweka steji za kukaa watu, mkifanya hivyo mtakuwa mmemaliza na tunafahamu miundombinu ya michezo ina umuhimu wake.
"Tanzania inafikiriwa kwenye michuano mikubwa ya kimataifa sio kwamba inapendelewa bali kwa kuwa inakidhi vigezo, kwa hiyo lazima tuhakikishe tuna vigezo kuanzia sasa mpaka 2027,"amesema.
Ameongeza taarifa alizonazo kuna viwanja vitakavyoteuliwa kwa sababu vina nyasi za kupandikiza na vingine vina majani yasiyp ya kupandikiza."Kwa hiyo ni ninyi muamue mnataka majani ya aina gani ili na ninyi mkidhi vigezo. Niwapongeze wasanifu, niwapongeze wachoraji, nimppngeze ofisa ardhi, uwanja mzuri, mkubwa," amesema.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akiwa sambamba na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Shaka Hamdu Shaka wakifurahi baada ya kpata maelezo mafupi kupitia mchoro wa uwanja wa Mpira wa Magogo kutoka kwa Mkadiriaji Majengo wa Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam,Geofrey Nyaluke baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa uwanja huo leo Septemba 4,2022 unaojengwa ndani ya Halmashauri ya Geita ambao ujenzi wake kwa awamu ya kwanza unaendelea kwa kasi kubwaMAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi kupitia mchoro wa uwanja wa Mpira wa Magogo kutoka kwa Mkadiriaji Majengo kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam,Geofrey Nyaluke baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa uwanja huo leo Septemba 4,2022 unaojengwa ndani ya Halmashauri ya Geita ambao ujenzi wake kwa awamu ya kwanza unaendelea kwa kasi kubwa.Pichani kushoto anaeshudia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Shaka Hamdu Shaka.Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akionesha sehemu/eneo ya mchoro ya uwanja huo itakapopandwa miti ikiwa ni sehemu ya kulinda/kutunza mazingira MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa uwanja huo wa Magogo leo Septemba 4,2022 unaojengwa ndani ya Halmashauri ya Geita ambao ujenzi wake kwa awamu ya kwanza unaendelea kwa kasi kubwa.Pichani kushoto anaeshudia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Shaka Hamdu Shaka na kulia ni Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Geita Said Kalidushi.PICHA NA MICHUZI JR-GEITA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...