WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na uwekezaji Mudrick Ramadhan Soragha amesema kutokana na kuendelea kukua kwa visiwa vya Zanzibar kwa kasi na kuendelea kwa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo, kunahitajika kuwepo kwa wataalam wa usimamizi wa miradi ili kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inayoendelea kujengwa inakamilika kwa wakati ili kuendelea kukuza uchumi wa visiwa hivyo nankuwalete wananchi maendeleo.
Waziri Soragha ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia umuhimu wa kongamano la taasisi ya Usimamizi na uendeshaji wa Miradi -PMI- lenye lengo la kutoa mafunzo ya usimamizi wa miradi kwa wasimamizi wa miradi wa taaluma mbalimbali visiwani humo, kongamano linalotarajia kufanyika Oktoba 20-21 visiwani humo.
Waziri Soragha amesema mara baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo ya wasimamizi wa miradi yatakayotolewa kwenye kongamano hilo, serikali na nchi inatarajia kutakuwa na miradi iliyokwama kutokana na sababu mbalimbali.
Rais wa Bodi ya Taasisi ya usimamizi na uendeshaji wa miradi tawi la Tanzania Ella Naiman na wajumbe wa bodi ya PMI, Daniel Materu na Kheri Mbiro wamesema baadhi ya miradi inakwama kukamilika kwa sababu wasimamizi wa miradi hiyo wanakuwa hawana elimu ya ubobezi wa usimamizi wa miradi.
Kongamano la wasimamizi wa miradi litafanyika Oktoba 20-21 visiwani Zanzibar na mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarajiwa kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman.
Kongamano hilo limedhaminiwa na CRDB, TIGO, serikali ya Zanzibar na HEBO Consult kwa kushirikiana na Deloitte (Tanzania), Miundo Misingi Hub (Kenya) na HEBO Consult (Tanzania).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...