Na.Khadija Seif Michuzi Tv

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Hassan Babu amezipongeza klabu za mchezo wa Gofu kwa kukuza,kuwapa hamasa na kuendeleza vipaji vya Vijana wadogo katika Mchezo huo.

Akizungumza katika Sherehe ya ufungaji wa Shindano la "TPC Open 2022" lililofanyika kwa siku tatu klabuni hapo Babu amesema,amefurahishwa kuona watoto wanaojitokeza kuucheza mchezo huo wanaendelea kuwa wengi kuanzia umri wa miaka 8 Hadi miaka 15.

"Nilifikiri mchezo huu huchezwa na watu matajiri lakini nimeshuhudia watu wa vipato vyote wakicheza mchezo huu watoto, vijana,wazee wote wanashiriki mchezo huu ".

Kwa Upande wake mshindi wa jumla wa shindano hilo Isiaka Daudi kutoka Lugalo Gofu Klabu amewashukuru wadhamini wa shindano hilo Benki ya CRDB,na amewaomba wachezaji wenzake waliofanya vibaya wajiaandae kwa ajili ya mashindano yajayo.

Shindano la TPC Open 2022,limemalizika siku ya jana,ambapo zaidi ya Wachezaji 90 kutoka vilabu mbalimbali wameshiriki shindano hilo,huku mshindi wa Jumla akiwa ni Isiaka Daudi wa Lugalo Gofu Klabu kwa Mikwaju 144 akifatiwa na Ali Mcharo wa TPC Moshi Mikwaju 145,ambapo kwa upande wa Wanawake Neema Olomi ameshika nafasi ya kwanza kwa wanawake kwa mikwaju 151 na kwa upande wa watoto Aladini Rashid akishika nafasi ya kwanza kwa mikwaju 166,huku kwa Wachezaji wakulipwa Frank Mwinuka wa Lugalo Gofu Klabu akiibuka kifua mbele kwa mikwaju 140.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Hassan Babu akikabidhi kombe kwa Mshindi wa jumla ya mikwaju 144 Daudi Isihaka kutoka klabu ya lugalo gofu pembeni Nahodha wa klabu ya lugalo gofu Meja Masai Mara baada ya kumalizika kwa Shindano la TPC OPEN 2022 Lililofanyika Mkoani Kilimanjaro

 Picha ya pamoja kati ya washindi wa Shindano la TPC OPEN 2022 pamoja na Nahodha wa timu ya wanaume ya klabu ya lugalo mara baada ya kumalizika kwa Shindano hilo lililofanyika Mkoani Kilimanjaro wadhamini wakiwa benki ya crdb.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...