Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, asemesema kuwepo na kuendelezwa mashirikiano mazuri baina ya Serikali ya Australia na Zanzibar ni muhimu katika kuzitumia ipasavyo fursa za kiuchumi na kuendeleza utalamu wa fani mbali mbali.

Mhe. Othman ameyasema hayo ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar, alipokutana na Balozi wa Austalia nchini Tanzania Luke Williams, aliyefika kwa ajili ya mazungumzo kuhusiana na masuala mbali mbali ya mashirikiano baaina ya nchi hizo mbili.

Mhe. amesema, Austarlia ni nchi iliyopiga hatua katika masuala mbali mbali yakiwemo ya utaalamu kwenye fani tofauti ikiwemo sheria na taaluma nyenginezo na kwamba Zanzibar inaweza kujifunza na kufanika sana na ushirikano kutoka nchi hiyo.

Aidha Mhe. Makamu amesema Zanzibar imekabiliwa na changamoto kubwa za mabadiliko ya Taibia nchi ambapo hivi sasa sehemu kadhaa za visiwa vya Zanzibar tayari zimeathirika kwa maji kuathiri ardhi zikiwemo za kilimo na makaazi ya watu jambo ambalo linahitaji msaada wa kiufundi ili kujijengea uwezo katika kupamba na tatizo hilo.

Mhe. Makamu amesema kwamba pia kuna haja ya nchi hizo kuangalia uwezekano wa kushirikiana katika kukabiliana na tatizo la kudhibiti ukataji miti holela kwa kuwa ni suala linaloathiri sana mazingira ikiwa ni pamoja na kuwepo mashirikiano katika kutunza mazingira ya bahahari ili yasiendelea kuharibika.

Aidha amesema pia aneo jengine la kuangalia mashirikiano ni pamoja na na kuwaendelea wafugaji nyuki wadogo wa Zanzibar hasa kwa vile nchi ya Austalia inauwezo mkubwa wa kitaalamu na uzoefu katika uzalishaji wa asali kupitia ufugaji nyuki.

Amesema kwamba kufanya hivyo itakuwa ni fursa muhimu ya kuwasaidia wazanzibari iwapo nchi hiyo itaamua kuwasaidia na kuwaendelea wafugaji wadogo wa nyuki waliopo Zanzibar ikiwa ni jitihada za kuwawezesha kuzalisha asali bora kwa wingi kwa njia ya kisasa inayoweza kukuza soko la Zanzibar la bidhaa hiyo.

Naye Balozi wa Australia nchini Tanzania Luke Williams, pamoja na mambo mengine ameshukuru mashirikiano makubwa yaliyopo baina ya nchi yake na Tanzania na hasa Zanzibar na kuahidi kwamba nchi yake ipo tayari kuendeleza ushirikiano katika maeneo mbali mbali zikiwemo kukabiliana changamoto za athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amesema kwamba watanzania wengi wamepata fursa za kimasomo kwa fani mbali mbali za elimu ya juu jambo mbalo linadhihirisha na kuendelea mashirikiano ya kitaaluma na mambo mengine mbali mbali ya kimaendeleo.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia), akifurahia jambo na Balozi wa Australia nchini Tanzania Luke Williams baada ya kumaliza mazungumzo yao rasmi huko ofisini kwa Makamu Migombani mjini Zanzibar leo tarehe 20.09.22. Balozi Luke alifika ofisi kwa Makamu kwa mazungumzo rasmi kuhusiana na mashirikiano kwenye maeneo mbali mbali . ( Picha na Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Kitengo cha Habari

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia), akipokea zawadi kutoka Balozi wa Australia nchini Tanzania Luke Williams baada ya kumaliza mazungumzo yao rasmi huko ofisini kwa Makamu Migombani mjini Zanzibar leo tarehe 20.09.22. Balozi Luke alifika ofisi kwa Makamu kwa mazungumzo rasmi kuhusiana na mashirikiano kwenye maeneo mbali mbali . ( Picha na Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Kitengo cha Habari

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia), akizungumza na Balozi wa Australia nchini Tanzania Luke Williams ofisini kwa Makamu Migombani mjini Zanzibar leo tarehe 20.09.22. Balozi Luke alifika ofisi kwa Makamu kwa mazungumzo rasmi kuhusiana na mashirikiano kwenye maeneo mbali mbali . ( Picha na Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Kitengo cha Habari

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia), akizungumza na Balozi wa Australia nchini Tanzania Luke Williams ofisini kwa Makamu Migombani mjini Zanzibar leo tarehe 20.09.22. kushoto ni Helen Williams ambaye ni Balozi Luke. Balozi huyo alifika ofisi kwa Makamu kwa mazungumzo rasmi kuhusiana na mashirikiano kwenye maeneo mbali mbali . ( Picha na Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Kitengo cha Habari.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (katikati), akiwa katika picha tya pamoja na Balozi wa Australia nchini Tanzania Luke Williams ofisini kwa Makamu Migombani mjini Zanzibar leo tarehe 20.09.22 baada ya kumaliza mazungumzo yao rasmi. Kushoto kwa Mhe. Makamu ni Helen Williams ambaye ni Balozi Luke. Balozi huyo alifika ofisi kwa Makamu kwa mazungumzo rasmi kuhusiana na mashirikiano kwenye maeneo mbali mbali . ( Picha na Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Kitengo cha Habari .



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...