Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
KLABU ya Lugalo ya mchezo wa gofu inatarajia kuandaa mashindano 'NMB CDF Troph 2022' yanayotarajia kufanyika Oktoba Mosi hadi 2 mwaka huu.
Mashindano hayo yatakayofanyika katika viwanja vya gofu Kawe Jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha klabu zote nchini.
Akizungumza Dar es Salaam Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema mashindano hayo yatashirikisha makundi yote kuanzia wakubwa na watoto (Junior).
"Licha ya kuwepo kwa klabu zote, pia timu kutoka Malawi na viongozi waandamizi wa Jeshi la hili akiongozwa na Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo watashiriki mashindano haya makubwa kwa nchi hii."
Mashindano ya mwaka huu yatakuwa na mvuto kutokana na idadi kubwa ha washiriki ambao wamejisajili.
" Tunaamini mashindano haya ya mwaka huu yatakuwa na mvuto kutokana na idadi ya washiriki na maboresho yaliyofanywa na mdhamini NMB.
Nahodha wa Klabu hiyo, Meja Japhet Masai amesema wachezaji wote walioalikwa wataanza kucheza siku ya Ijumaa kwa 'mapro' wote kucheza kuanzia asubuhi na kwa wale wachezaji wa ridhaa watacheza siku ya Jumamosi na kwa ujumla mashindano yatakuwa ya siku mbili tu.
Aidha ameeleza kuwa mashindano hayo yatakuwa ya wazi kwa wachezaji kucheza kwa mfumo wa close na neti.
Upande wa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalum kutoka NMB ambao ndiyo wadhamini, Getrude Malliya amesema wameamua kudhamini mashindano hayo hili kuhakikisha mchezo huo unafika mbali.
"Tunafahamu kuwa mashindano haya yatafanyika chini ya uongozi mpya wa Mkuu wa Majeshi Tanzania na tukaona tuendelee kuwa wadhamini na kutoka kiasi cha shilingi milioni 25."
Katika mashindano hayo mgeni rasmi anatarajia kuwa Mkuu wa Majeshi na Ulinzi nchini, Jenerali Jacob Mkunda ambaye pia ni mlezi wa klabu ya Lugalo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya kutangaza udhamini wa Benki ya NMB wenye thamani ya Sh. Mil. 25 wa mashindano ya gofu ya Mkuu wa Majeshi ‘NMB CDF Trophy 2022’ yatakayofanyika Oktoba 1 na 2 kwenye viwanja vya Gofu Lugalo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalum Benki ya NMB, Getrude Mallya
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalum Benki ya NMB, Getrude Mallya (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Mil. 25 Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo (katikati), kwa ajili ya mashindano ya gofu ya Mkuu wa Majeshi ‘NMB CDF Trophy 2022’ yatakayofanyika Oktoba 1 na 2 kwenye viwanja vya Gofu Lugalo. Kulia ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Maalum, Hildegard Mng’ong’oni
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...