Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Vyombo vya Habari, Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-Tanzania), imezundua ripoti ya mwenendo wa vyombo vya habari nchini mwaka 2015/2021.

Akizungumza wakati uzinduzi wa ripoti hiyo leo, Septemba 10, 2022 Makamu Mwenyekiti wa Misa Tanzania, James Malenga amesema masuala ya kisheria ndiyo yaliyoangaziwa katika ripoti hiyo.

"Ripoti hii inahusu mambo mbalimbali kuhusu tasnia ya habari ikiwemo sheria, madhira waliyokutana nayo waandishi wa habari na mazingira kwa ujumla ya Vyombo vya habari," amesema.

Kwa mujibu wa Malenga, ripoti hiyo imeonyesha changamoto za kisheria ikiwemo ya Huduma za Habari na Makosa ya Mtandao.

Mathalan, sheria ya Huduma za Habari amesema ina changamoto kadhaa, akifafanua kipengele kilichompa mamlaka waziri husika kufungiwa vyombo vya habari.

Meneja wa Miradi kutoka taasisi ya Internation Media Support ambao ndiyo wasimamizi wa mradi huo, Fausta Busokwa amesema uzinduzi wa ripoti hiyo umelenga kuongea uelewa wa wadau kuhusu uboreshaji wa sheria za Habari.

"Tunalenga kuzifanya sheria zetu ziwe zinahamasisha uhuru wa kujieleza na kutoa taarifa," amesema.

Shilinde Sued ni miongoni mwa waandishi wa ripoti hiyo, amesema ndani ya ripoti hiyo Sheria ya Makosa ya Mtandao imehusishwa na changamoto zake.

"Vitu tulivyoangalia ni kwa namba gani sheria hii inaweza kutekelezeka bila kuathiri utendaji wa waandishi wa habari," amesema.


  Makamu Mwenyekiti wa Misa Tanzania, James Malenga akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo na kueleza kuwa  masuala ya kisheria ndiyo yaliyoangaziwa katika ripoti hiyo, Leo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Miradi kutoka taasisi ya Internation Media Support ambao ndio wasimamizi wa mradi huo, Fausta Busokwa akizungumza wakati wa uzinduzi huo na kusema kuwa uzinduzi wa ripoti hiyo umelenga kuongeza uelewa wa wadau kuhusu uboreshaji wa sheria za Habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...