Moja ya changamoto kuwa kuhusu afya ya uzazi Nchini Tanzania ni kuwa watu wengi hawana elimu ya kutosha, hasa vijana ndio maana matukio kama ya mimba zisizotarajiwa yamekuwa ni kawaida kutokea.

Siyo kwa vijana tu, bali hata watu wengi wazima suala hilo ni changamoto kubwa kwao.

Matukio ya ukatili yanayoendelea kutokea katika jamii zetu sehemu mbalimbali Nchini yanatoa picha jinsi hali inapozidi kuwa mbaya, na takwimu nyingi zinaonesha kuwa waathirika wakubwa ni Wanawake.

Zipo jitihada za Serikali na Mashirika mbalimbali zimefanyika kutoa elimu lakini upande wa pili matukio ya ukatili dhidi ya Wanawake yameendelea kwa wingi.

Pamoja na yote yanayoendelea na uwepo wa Sheria kadhaa za kulinda na kutetea haki ya afya na utu wa Mwanamke lakini inapotokea matukio kama ya ubakaji yanayosababisha mimba zisizotarajiwa, hata kama mtuhumiwa atachukuliwa hatua za kisheria, bado Sheria haimpi mwathirika nafasi ya kurejea katika Ulimwengu wake ilivyokuwa mwanzo

Mfano mwanamke kabakwa au katembea na ndugu yake wa damu, baada ya muda anabainika kuwa na ujauzito, ikitokea hana mpango wa kuendelea na ujauzito huo hawezi kufanya hivyo kwa kuwa Sheria haimruhusu kuitoa.

ATHARI ZA KISAIKOLOJIA 

Katika mazingira ya kawaida mwathirika anapobainika kuwa na mimba, ni wazi kuwa kama hana mpango wa kuitunza, akibaki nayo inaweza kuwa na athari kubwa kisaikolojia na imetokea mara nyingi, vyombo vya habari vikiripoti.

Atakapokuwa anaona ujauzito unakuwa ndivyo ambavyo atakuwa anaumia na kuathirika zaidi kisaikolojia, wakati mwingine waathirika wa aina hiyo ndio wale ambao unasikia wamehusika katika kuua watoto wao au kuwatelekeza au kuwatupa wakiwa bado wadogo.

NINI KINAFANYIKA KUOKOA JAHAZI?

Tanzania ilisaini Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu - Mkataba wa Nyongeza wa Haki za Wanawake Barani Afrika ukijulikana kama MKATABA WA MAPUTO au MAPUTO PROTOCAL.

Mkataba huo ulitungwa kuwa sehemu ya nyongeza ya Mkataba wa Haki za Binadamu na Watu wa Mwaka 1981.

Ujio wa nyongeza ya mkataba huo ulitokana na kuonekana kuna mambo yanakoseka kuhusu haki za Wanawake, ambapo ulisainiwa Julai 2003 na ukaanza kutumika mwaka 2005, lakini kwa Tanzania ulianza kutumika mwaka 2007.

IBARA YA 14 (2c) YA MKATABA WA MAPUTO

Tanzania baada ya mkataba huo mrngi yalifanyiwa kazi lakini katika suala hilo la kulinda Wanawake wanaopata ujauzito kwa njia ya ukatili au pasipo kutarajia kama inavyoelezewa katika IBARA YA 14 (2c) ya mkataba huo wa Maputo.

Kipengele hicho kinahusu masuala ya afya ya uzazi hasa katika kutoa mwanya kwa Mwanamke kutolewa/kutoa mimba pale anapokabiliana na mazingira kadhaa ambayo yanaweza kuwa hatarishi kwake.

Kwa Tanzania, Sheria zinaeleza utoaji mimba ni kosa lakini inaruhusiwa kwa masharti ya kuwa ujauzito unahatarisha afya au maisha ya mama.

Lakini katika MKATABA WA MAPUTO kuna vipengele vinavyotoa uwanja mpana wa mazingira ya utoaji mimba pale kunapokuwa na uhitaji huo, na baadhi ya Nchi ambazo nazo zimesaini mkataba huo zimechukua vipengele vingine kadhaa.

USHAURI

Kuna mazingira mengi ambayo yanaacha maswali kwa jamii mfano, mimba za utotoni, mimba zinazotokana na kubakwa, vipi kama uwezo wa kiuchumi hauruhusu?

Maswali yako mengi ambayo yanaweza kutokana na ujauzito kupatikana kutokana na mazingira ambayo si rafiki na Sheria hazimpi nafasi Mwanamke kujiamulia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...