Na Mwandishi Wetu, Michuzi

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limesema katika kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia katika Mkoa huo wamefanikiwa watuhumiwa wawili kwa kosa ubakaji na kwamba watuhumiwa hao baada ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria wamehukumiwa kifungo cha miaka 80 kwa wote wawili.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema watu waliokamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya ubakaji ni Paul Hilonga (60) mkazi wa Karatu pamoja na Erasto Sias(24) mkazi wa Qurus ambaye anatuhimiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka name.

Kamanda Masejo amesema watuhumiwa hao baada ya kukamatwa walipelekwa kwenye vyombo vya sheria na watuhumiwa hao ambapo Hilonga anatumikia kifunga cha miaka 50 jela na Sias anatumikia kifungo cha miaka 30.

Katika hatua nyingine, Kamanda Masejo  amekutana na askari katika wilaya ya Karatu na kubainisha kuwa lazima wakubali ukweli kuwa kuna baadhi yao wanakwenda  kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi.

Hivyo amewaambia  askari kuwa hato sita kuchukua hatua kwa askari wasio zingatia nidhamu haki weledi na uadilifu kwa atakaye Kwenda kinyume na mwendo mwema wa Jeshi la Polisi.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...