Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linamshikilia Reginald Ambros maarufu kwa jina la Amsi (42) ambaye ni mkazi wa Endabashi akiwa na vipande viwili vya jino la tembo alivyokuwa amevifunga kwenye boksi.

Akitoa taarifa hiyo leo Septemba 12,.2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP Justine Masejo amesema jeshi hilo limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Septemba 10,2022 kutokana na taarifa za wananchi wenye mapenzi mema na rasilimali za nchi ambazo zimekuwa zikiliingizia pato taifa ikiwa ni pamoja na fedha za kigeni.

Kamanda Masejo amesema kwamba baada ya taarifa Polisi walimfuatilia na ndipo saa nane usiku wa tarehe hiyo wakafanikiwa kumkamata na uchunguzi wa awali umebaini amekuwa akijihusisha na matukio ya biashara haramu ya uuzaji wa nyara za Serikali huku akifafanua kwa sasa wanaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo ilikupata mtandao mzima.

Katika hatua Kamanda Masejo ameeleza kuwa jeshi hilo lilifanikiwa kukamata jumla ya lita 1,480 za pombe haramu aina ya gongo, mitambo 80 ya kutengeneza ombe hiyo Pamoja na watuhumiwa 62 ambao wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...