Meneja TARURA Mkoa wa Pwani Mhandisi Leopold Runji wakibadilishana mikataba na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wakandarasi wanawake Tanzania Mhandisi, Debora Sengati wakishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge leo Septemba 8, 2020.
Mkuu wa Mkoa w Pwani, Abubakari Kunenge akizungumza kwenye hafla ya utiaji wa saini wa mikataba 40 yenye thamani ya Sh.Bil.10.85 iliyofanyika Wilayani Kibaha Septemba 8, 2022.
Meneja TARURA Mkoa wa Pwani Mhandisi Leopold Runji akielezea namna watakavyo isimamia  mikata hiyo ya ujenzi na matengenezo ya barabara.
Kutoka kushoto ni Meneja wa TARURA Mkoa wa Pwani  Mhandisi, Leopold Runji, RAS Zuwena Omary akifuatiwa na RC Kunenge, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani  Ramadhan Maneno na Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhandisi Martin Ntemo waliosimama ni baadhi ya wakandarasi wakiwawakilisha wenzao wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushuhudia utiaji wa saini wa mikataba 40 yenye thamani ya Sh.Bil.10.85.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wakandarasi wanawake Tanzania Mhandisi, Debora Sengati kutoka Kampuni ya ULM Investment Co.Limited akizungumza na waandishi hawapo pichani.

Na Khadija Kalili, KIBAHA
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amewataka wakandarasi wa ujenzi wa barabara ambao wamehudhuria hafla ya utiaji saini mikataba 40 ya matengenezo ya barabara kwa mwaka 2022-23 TARURA Mkoa wa Pwani kuanza kazi mara moja kama jinsi mikataba yenu inavyojieleza.

RC Kunenge amesema hayo leo asubuhi Septemba 8, 2022 wakati akishuhudia utiaji wa saini wa mikataba 40 yenye thamani ya Sh.Bil.10.85 sawa na asilimia 60 ya kazi zote kwa kipindincha mwaka 2022/23 hafla hiyi imefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye jengo la Mkuu wa Mkoa Wilayani Kibaha.

"Mkoa wa Pwani una mtandao wa barabara wenye urefu wa KL.6,441,55 ambapo wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) inasimamia KM.1,387.98 na wakala wa barabra za Vijijini na Mjini (TARURA) inasimamia KM.5,053.57 kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya bara bara katika Mkoa wa Pwani" amesema RC Kunenge.

RC Kunenge amesema kuwa mikataba hii itahusisha matengenezo ya barabara ya kiwango cha lami, kiwango cha changarawe, ujenzi wa madaraja na ufunguzi wa barabara mpya kabisa na hadi leo Mkoa umepokea Bil.2.1 kwa ajili ya kazi hizo hivyo wakandarasi mfanye kazi kwa juhudi."amesema RC Kunenge.

Ongezeko la bajeti hii kwa TARURA linakwenda kuongeza urefu wa barabara za lami kutoka kilometa 74 za sasa mpaka kufikia kilometa 82 ambazo ni sawa na asilimia 10 pia barabara za changarawe zenye urefu wa Kilometa 198.06 zitajengwa na kufanya ongezeko la asilimia 19 kutoka Kilometa 816.62 hadi kufikia Kilometa 1,014.68 ifikapo June 2023, vilevile makaravati 162 na madaraja manne yatajengwa,amesema RC Kunenge.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani ametoa rai kwa menejimenti ya TARURA Mkoa na Mameneja wa Wilaya kusimamia ipasavyo miradi ya barabara ili kuhakikisha thamani ya fedha iweze kuonekana kwa kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ubora na muda uliokusudiwa kimkataba.

"Natoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani kuwa walinzi wa vifaa vitakavyotumika katika ujenzi ili wananchi wasiwe chanzo cha kuhujumu au kuharibu miundombinu ya barabara kwani serikali inatumia fedha nyingi kuhakikisha barabara zinaboreshwa Agosti14 mwaka huu Jijini Dodoma Rais Samia Suluhu Hassan aliagiza Halmashauri zote nchini ziweze kutenga fedha kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu katika maeneo ya kimkakati kusaidia bajeti ya TARURA.

Meneja wa TARURA Mkoa wa Pwani Mhandisi Leopold Runji amesema kuwa mikataba hii iliyosainiwa leo inakwenda kuboresha barabara kutokana na uwekezaji mkubwa wa viwanda mkoani Pwani.

"Ni dhahiri tunahitaji fedha nyingi katika kuimarisha miundombinu ya barabara hivyo ni matumaini yetu kuwa wewe RC ukiwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya barabara ya mkoa utasaidiana na TARURA Mkoa wa Pwani katika kutafuta fedha za ujenzi wa barabara za kimkakati zinazo unganisha mji wa Kibaha na vituo vya reli ya SGR (Sogana Ruvu 21 Km), maeneo ya uwekezaji SINO-TAN na bandari kavu ya kwala yenye urefu wa Km.5."

Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Chama Cha Wakandarasi wanawake Tanzania nzima Mhandisi Debora Sengati ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya ULM Investment Co.Limited ameshauri wakandarasi wenzake kutimiza ahadi ya ujenzi wa barabara kulingana na mikataba yao inavyosema samvamba kukamilisha kazi zao kwa wakati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...