Uchaguzi uliofanyika kwenye Jumuiya ya wazazi, Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi na umoja wa Wanawake wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma umetoa sura mpya katika nafasi mbalimbali zikiwemo nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya hizo.

Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Acheni Mwinsheshe Maulidi alisema kuwa uchaguzi katika ngazi ya jumuiya hizo tatu ulienda vizuri kwa wajumbe kuwachagua wanachama wenzao wenye Imani nao ya kuwatumikia katika chama.

Aidha Maulidi alidai uchaguzi wa jumuiya hizo ulifanyika kuanzia tarehe 23 mwezi huu na kumalizikia tarehe 25 mwezi huu katika ukumbi wa shule ya sekondari Nasuli ambapo wajumbe kutoka katika matawi ya kata 21 ya wilaya ya Namtumbo walihudhuria uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo Paul Tenela Katobesi alisema nafasi ya mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi imechukuliwa na George Luambano kutoka kwa Ramadhan Abbdallah.

Katobesi alidai katika nafasi ya uenyekiti wa umoja wa vijana nafasi moja iliombwa na George Luambano na Ahmadi Mpoma ambapo George Luambano alijizolea kura 230 na Ahmadi Mpoma alipata kura 130 huku idadi ya wajumbe ilikuwa 378 kura zilizopigwa zilikuwa 378 kura halisi 361 zilizoharibika 17.

Katika nafasi ya umoja wa wazazi nafasi ya uenyekiti imechukuliwa na Lukas Ching”ang”a kwa kupata kura 180 huku wapinzani wake Maneno Wami alipata kura 179 na Matrida chale aliyekuwa akitetea kiti hicho akipata kura 65.

Hata hivyo katika umoja wa wanawake nafasi ya uenyekiti imechukuliwa na Nuru Omari Ndimbo kwa kupata kura 217 na kuwashinda wagombea wenzake Ritha Nchimbi aliyepata kura 29 na Sheira Ured Mgoda aliyepata kura 79ambapo mwenyekiti wa awali alikuwa Martha Nikata ambaye hakubahatika jina lake kurudishwa ili aweze kuingia katika kutetea kiti chake hicho.

Chaguzi hizo za jumuiya zilichagua pia wajumbe wa mikutano mikuu wilaya na taifa ambapo upande wa umoja wa vijana Zuberi Nikata alichaguliwa mjumbe wa mkuutano mkuu wa chama na Jordani Shawa alichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa chama wilaya.

Anjela Omari Maputa alichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa UWT taifa na ndugu Shaibu Majiwa alichaguliwa kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa wazazi Taifa na ndugu Anjela alichaguliwa katika nafasi ya mkutano mkuu wa mkoa. Uchaguzi huo wa chama utaendelea siku ya tarehe 2 mwezi oktoba mwaka huu katika nafasi ya uenyekiti wa chama wilaya ,katibu mwenezi wa chama wilaya ,wajumbe wa Halmashauri kuu ya chama ,wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya na mwakilishi wa mkutano mkuu taifa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...