Na Said Mwishehe,Michuzi Blog 
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Profesa Francis Matambalya ameeeleza kwamba taasisi hiyo imeandaa  mdahalo wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika Septemba 20,2022 jijini Dar es Salaam ukiwa na lengo kuangazia changamoto na namna bora ya kuendelea kudumisha amani kupitia demokrasia ya vyama vingi nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Septemba 19,2022 jijini Dar es Salaam Profesa Matambalya amesema mdahalo huo utakaoshirikisha makundi mbalimbali wakiwemo wanasiasa wa vyama mbalimbali na utaongozwa na Jaji mstaafu Joseph Warioba
"Tutakuwa na wadau mbalimbali wakiwemo wa vyama vya siasa na mdahalo wetu pamoja na mambo mengine utajadili wajibu wa pamoja wa wadau wa kisiasa katika kulinda na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi nchini,"amesema.
Amefafanua kuwa mdahalo huo utafanyika kwa siku moja kesho Jumanne Septemba 20, 2022 na utaongozwa na Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba na kwamba lengo kubwa la mdahalo huo ni mashauriano ya kubadilishana mawazo ili kuimarisha maarifa ya taaluma ya ujuzi na weledi wa kiuongozi katika kukuza na kulinda demokrasia ya vyama vingi hapa Tanzania.
Aidha amesema kwenye mdahalo huo pia kutakuwa na wawakilishi wa makundi mbalimbali yakiwemo ya wanasiasa, Bunge, Serikali na asasi za kiraia zinazosimamia makundi ya watu wenye ulemavu.
"Tutabadilisha mawazo na kujifunza kuhusu midahalo kama hii tulioifanya Zanzibar na Tanzania bara,"amesema na kuongeza watumia nafasi hiyo kuzungumzia sababu na historia ya kufanya mdahalo na walichojifunza kwa wenzeo wa Zanzibar na Tanzania Bara. 
"Na baada ya majadiliano kwenye mdahalo huo tutakuwa na majumuisho ya masuala mahsusi yatakayopewa uzito katika mdahalo huu utakaowashirikisha wageni kutoka Kenya na Uganda," amesisitiza.
Pamoja na mambo mengine miongoni mwa mambo yaliyobainika katika midahalo iliyofanyika Tanzania Bara na Zanzibar kwa nyakati tofauti ni mpasuko kati ya wanasiasa na vyama vya siasa nchini.
Ameeleza hivyo wameogopa mpasuko huo  ukiachwa unaweza kukugusa umma na kuleta matatizo, lakini utafiti tulioufanya umebaini bado kuna mshikamano wa wa Watanzania ukiachana na masuala ya vyama vya siasa.Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Prof. Francis Matambalya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi kuhusu mdahalo wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Septemba 20,2022 ulioandaliwa na Taasisi hiyo,ambao utawashirikisha wanasiasa na wadau mbalimbali wa siasa,ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.Kulia ni Naibu Mkuu wa fedha na utawala,Makongoro Gidai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...