Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi kupitia kikosi Cha kuzuia wizi wa mifugo (STPU) kimesema kuwa kimearisha ulinzi na kutoa elimu kwa wafugaji katika Kijiji cha msomera na kuwahakikishia wakazi wapya waliohamia katika wilaya ya Handeni kijiji cha msomera kuwa mifugo yao iko salama na kuwa taka kutoa ushirikiano kwa kikosi hicho ambacho kinashughulika na migogoro ya mifugo na wakulima ambapo hadi Ivi sasa zaidi ya mifugo elfu Tano imeshawasili Msomera.

Hayo yamesemwa leo  septemba 09, 2022 na kamanda wa Polisi  kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo (STPU) Tanzania kamishina msaidizi wa Polisi ACP SIMON PASUA alipofika katika wilaya ya handeni Kijiji cha msomera kushudia zoezi la kuhamisha mifugo kutoka mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Kwenda katika wilaya ya handeni mkoa wa Tanga na kusema kuwa zaidi ya mifugo elfu tano mia nne na tatu iliyotoka katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imewasili salama katika Kijiji cha Msomera wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga.

ACP PASUA amewambia wananchi katika Kijiji cha msomera kuwa wafugaji wanao wajibu wa kufurahia mazingira bora kwa shughuli zao za ufugaji na kilimo ambapo amesema msomera ni eneo zuri kwao kama wafugaji na kuwataka wafuate matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji katika eneo hilo.

Nao baadhi ya wafugaji wa jamii ya kimasai waliohamia katika wilaya ya handeni katika Kijiji cha msomera wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuwajalia wafugaji na kuwawekea mazingira bora na rafiki katika shughuli za ufugaji.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...