Wanging’ombe
Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe Lauteri Kanoni ameagiza wakuu wa shule na maafisa elimu katika wilaya hiyo kuwasimamia wasaidizi wao (walimu) wasiweze kutoroka kwenye vituo vyao vya kazi wakati wa muda wa muajiri wao na kwenda kutafuta fedha za kujiongezea vipato kwa kuwa serikali imeshatoa fedha kwa ajili yao.
Ametoa agizo hilo wakati akizindua vitabu vya mwongozo wa kufundishia na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi ambapo amesema kuwa Bado kuna changamoto ya utoro kwa wanafunzi na walimu.
“Sio utoro tu kwa wanafunzi upo utoro na kwa walimu kwa hiyo maafisa elimu,wakuu wa shule mkawasimamie wasaidizi wetu wasitoroke watimize dajibu wao,sasa hivi serikali imeshamwaga mahela tena wala sio ya UVIKO ila ni ya kwetu sisi wenyewe”amesema Kanoni
Vile vile ameelekeza shule zilizopewa jukumu la kujenga madarasa ziweze kuanza kufanya maandalizi ya kutosha kwa kuwa tayari serikali imetoa siku 75 kwa wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...