Na.Abel Paul wa Jeshi la Polisi,Ikwiriri Rufiji Pwani
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vimefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumia saba wamatukio ya uchochezi wa migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika kitongoji cha Usimbe kata ya Maparoni Wilaya ya kibiti mkoa wa Pwani iliyotokea tarehe agosti 30 mwaka huu.
Akitoa taarifa hiyo September 10 2022 alipofika katika Kata ya Maparoni wilaya ya kibiti kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Nchini kamishina msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua amesema Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakata watuhumiwa saba wa matukio ya uchochezi baina ya wakulima na wafugaji katika Kata ya Maparoni wilaya ya kibiti mkoa wa Pwani.
Pasua amesema watuhumiwa hao bado wanashikiliwa na Jeshi hilo huku akisema kuwa majina yao yanahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi nakubainisha kuwa wamehojiwa na kukiri kufanya matukio hayo kama iliyoonekana katika video iliyosambaa katika baadhi ya mitaandao ya kijamii I kilionyesha baadhi ya wakulima wakiwakimbizwa na kuchapwa viboko na baadhi ya wakulima wakulima katika Kata ya Maparoni wilaya ya Rufiji.
Kamanda Pasua ameeleza kuwa watuhumiwa wote watafikishiwa katika vyombo vya sheria pindi upelelezi utakapo kamilika kujibu tuhuma zinazowakabili.
Sambamba na hilo ACP Pasua ameendelea kuwaeleza waandishi wahabari kuwa Jeshi la Polisi linawataka walewote waliowalihusika katika tukio hilo baya wajisalimishe katika vituo vyao Polisi kabla wajakumbana na mkono wa dora.alisema Pasua
Hata hivyo ameongeza kuwa kuna taarifa za baadhi ya wafugaji wanao hamisha mifugo kutoka eneo moja kwenda eneo jingne kwa lengo la kutafuta malisho ambapo amesema vitendo hivyo vimekuwa chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji katika maeneo mengi hapa nchini ambapo amewataka kufuata matumizi bora ya ardhi.
Nao baadhi ya wahanga katika tukio hilo wameliomba Jeshi la Polisi hususani kikosi kinachoshughulika na migogoro baina ya wakulima na wafugaji kuongeza kasi ya kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...