Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Consolation Medicare Severian
Christopher ambao ni wasambazaji wa vifaa tiba akizungumza wakati wa zoezi hilo na kueleza kuwa wamedhamini na kushiriki
zoezi hilo katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za
afya.
Mtaalam wa afya kutoka Moraf Pharmacy ambao ni
wasambazani wa dawa na vifaa tiba kutoka nchini India Nickson Byarushengo akizungumza wakati wa zoezi hilo na kueleza kuwa wamedhamini na kushiriki zoezi hilo kwa kuwawezesha wananchi dawa mbalimbali
pamoja na kuwajengea uelewa wa matumizi ya dawa hizo kwa wagonjwa.
· * Wadau waeleza utayari wa kushirikiana na Serikali katika kuboresha sekta ya afya
WANANCHI wa Manispaa ya Temeke wamejitokeza kwa wingi na kupata huduma za afya za kibingwa zilizotolewa bure bila malipo na menejimenti ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa na mkuu wa Wilaya ya Temeke pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya afya wakiiwemo Consolation Medicare, Moraf Phamarcy pamoja na MDH.
Akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi hilo la Temeke Afya check lililoanza leo katika viwanja vya hospitali hiyo Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa zoezi hilo na Daktari bingwa wa kinywa na meno Dr. Tusibilege Mwakasungule amesema katika zoezi hilo wameshirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi ili kuwarahisishia wananchi katika kupata huduma hizo pamoja na kuhamasisha wananchi kupima afya zao mara kwa mara.
Amesema, zoezi hilo litafanyika kwa siku tatu na wameshirikiana na wadau mbalimbali ambao wamechanga vifaa pamoja na wataalam ambao wanahudumia wananchi wa Temeke kupitia zoezi hilo la Afya Check.
‘’Ni mara ya pili tunafanya zoezi hili kwa kushirikiana na wadau ambao wamekuwa wakitoa dawa, vifaa tiba pamoja na wataalam….Mwitikio ni mkubwa kwa masaa manne tayari wagonjwa 200 wamapata huduma tunategemea kufikia lengo la kuwafikia wagonjwa 1500 kwa siku tatu litatimia.’’ Amesema.
Dr. Twisibilega amesema huduma zitakazotolewa bure malipo kuanzia tarehe 9 hadi 11 Setemba mwaka huu ni pamoja na magonjwa ya wanawake na uzazi, magonjwa ya watoto, magonjwa ya pua, koo na masikio, magonjwa ya mifupa na majeraha ya ajali, magonjwa ya njia ya mkojo na tezi dume, magonjwa ya sukari, figo, shinikizo la damu, magonjwa ya macho na uoni hafifu, magonjwa ya kinywa na meno, upasuaji mkubwa na mdogo pamoja na magonjwa ya akili.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Consolation Medicare Severian Christopher ambao ni wasambazaji wa vifaa tiba amesema, wamedhamini na kushiriki zoezi hilo katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha huduma za afya kupitia hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke.
Amesema taasisi za namna hiyo zina mchango mkubwa sana katika kuhamasisha jamii juu ya upimaji wa afya mara kwa mara.
‘’Utaratibu wa kupima afya mara kwa mara utaokoa maisha ya watanzania wengi kwa kuwa upimaji wa afya hauzingatiwi..Tumekuja hapa kushiriki zoezi hili kwa kutoa huduma na kutangaza vifaa vya kibingwa tunavyovisambaza.’’ Amesema.
Aidha amesema wapo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuboresha huduma za afya zinafanikiwa kwa kila mwananchi kufikiwa na huduma za afya za kibingwa.
Kwa upande wake mtaalam wa afya kutoka Moraf Pharmacy ambao ni wasambazani wa dawa na vifaa tiba kutoka nchini India Nickson Byarushengo amesema wamedhamini na kushiriki zoezi hilo kwa kuwawezesha wananchi dawa mbalimbali pamoja na kuwajengea uelewa wa matumizi ya dawa hizo kwa wagonjwa.
‘’Tunazitoa dawa hizi bure kwa wagonjwa zikiwemo za kinywa na meno na ubora wake utawafanya wagonjwa kuzinunua kwa matumizi.’’ Amesema.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...