Na Mwandishi Wetu - Singida
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameelekeza viongozi wanaosimamia ukarabati wa Chuo cha Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu Sabasaba, kuhakikisha gharama zinazotumika kununua vifaa pamoja na ubora wa vifaa vinavyotumika katika ukarabati huo uendane na thamani ya fedha zinazotumika.
Zaidi ya Shilingi milioni 800 zimetolewa kwa ajili ya Mradi wa ukarabati wa Chuo cha Marekebisho na Ufundi Stadi Sabasaba kwa Watu Wenye Ulemavu, mkoani Singida, kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.
Mhe. Waziri Ndalichako ametoa maelekezo baada ya kufanya Ukaguzi wa ukarabati wa chuo hicho ambapo amesisitiza ni muhimu ukarabati kuendana na thamani ya fedha kwa kuwa Ofisi hiyo kwa mwaka huu wa fedha inao mpango wa kujenga vyuo vipya kwa Watu wenye Ulemavu, kwa msingi huo umakini wa usimamizi wa matumizi ya fedha utawezesha ujenzi huo kuwa bora.
“Mhe. Rais amekuwa akisisitiza watendaji kuwa makini katika utendaji wetu kila senti ya serikali tuilinde, ili kuhakikisha fedha zinazotolewa zinakuwa na tija iliyokusudiwa”
Kwa upande wake Mkuu Mkuu wa chuo hicho Fatma Malenga, pamoja na Msimamizi wa Majengo kutoka DIT, Masunga Salum, wamemhakikishia Mhe. Waziri kuwa watayatekeleza maelekezo aliyoyatoa kwa wakati ili ujenzi huo ukamilike kama ilivyokusudiwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akikagua ukarabati wa majengo katika Chuo cha Marekebisho na Ufundi Stadi Sabasaba kwa Watu Wenye Ulemavu, mkoani Singida.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiongozana na wataalam wakati akikagua ukarabati wa majengo katika Chuo cha Marekebisho na Ufundi Stadi Sabasaba kwa Watu Wenye Ulemavu, mkoani Singida.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wanafunzi wenye Ulemavu baada ya kukagua ukarabati wa majengo katika Chuo cha Marekebisho na Ufundi Stadi Sabasaba kwa Watu Wenye Ulemavu, mkoani Singida.
Msimamizi wa Majengo kutoka DIT, Masunga Salum, (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako alipokuwa akikagua ukarabati wa majengo katika chuo cha Marekebisho na Ufundi Stadi Sabasaba kwa Watu Wenye Ulemavu, mkoani Singida.
Muonekano wa jengo mmoja wapo lililokaraba
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...