Na Avila Kakingo, Michuzi TV
KIWANDA cha kutengeneza dawa za tiba asili cha Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Mabibo jijini Dar es Salaam, kinatarajia kuanza kuzalisha dawa asili ndani ya mwaka fedha wa 2022/2023.
Na Zaidi ya Shilingi Bilioni mbili zinatarajiwa kuwekeza na Serikali ili kukamilisha ujenzi na usimikaji mitambo katika kiwanda hicho ambacho kitatengeneza dawa zinazotokana na miti dawa hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. Yunus Mgaya wakati akizungumza na Waandishi wa habari Septemba 6, 2022, katika Ziara ya Baraza la NIMR ya kukagua maendeleo ya ujenzi na usimikaji wa Mitambo katika kiwanda hicho.
Amesema kuwa NIMR Kwa kushirikiana na Serikali imefanikiwa kuingiza mitambo ya uzalisha kutoka nchini China; na kwamba wapo katika hatua za mwisho za usimikaji mitambo katika Kiwanda hicho.
Prof. Mgaya amebainisha kuwa mradi huo ni wakipekee kwa sababu ujenzi wa kiwanda hicho haujawahi pata ufadhili wa kusimika mitambo hiyo ya kutengeneza dawa asili NIMR.
"Tunashukuru sana kupewa hii fursa ya mitambo hii kusimikwa na NIMR na tuisimamie kwa sababu itaongeza uwezo wetu wa kufanya tafiti, hasa kwenye uzalishaji wa zile dawa tunazitumia kwenye utafiti." Amebfafanua Prof. Mgaya
Amesema dawa inapopasishwa au kufaulu kwenye utafiti na Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya dawa na Vifaa tiba (TMDA) na wakakubaliana na dawa hizo; ndipo uwezo wa kuzalisha dawa nyingi zaidi utakuwa wa uhakika.
Amesema kuwa dawa ili iingie kwenye soko lazima ipitie kwenye vigezo vya ubora na usalama na uthibitisho huo utakuwa unapita kwenye kiwanda hicho.
"Katika kiwanda hiki sisi tunaanzia kwenye mti porini, mti ambao tutatukwa tumeshaufanyia utafiti, tunauleta kwenye mitambo yetu hapa tunaichakata mpaka tunakuja kupata kidonge." Amesema Prof. Mgaya
Licha ya hayo Prof. Mgaya ameishukuru Serikali na Wizara ya Afya pamoja na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuchangia fedha za kuwezesha kufanyika uwekezaji huo mkubwa ili kuhakikisha maabara inakuwa na ukamilifu wa kutosha Kwa viwango stahiki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza NIMR Dkt. Andrew Kitua amesema kuwa uwekezaji mkubwa umeweka katika eneo la NIMR Mabibo kwa ajili ya kutengeneza dawa za asili ili kuweza Kuisaidia jamii ya kitanzania katika kujitibu maradhi mbalimbali yakiwemo yasiyoambukiza kwa kutumia dawa za asili.

Baadhi ya Mitambo iliyosimikwa katika kiwanda cha Dawa asili kilichopo NIMR mabibo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuanza kuzalisha dawa asili hapa nchini.
Mkurugenzi wa Kuratibu na Kukuza Utafiti NIMR, Dkt. Paul Kazyoba akifafanua jambo katika Ziara ya Baraza la NIMR ya kukagua maendeleo ya ujenzi na Usimikaji wa Mitambo katika kiwanda cha dawa asili kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Mitambo iliyosimikwa katika kiwanda cha Dawa asili kilichopo NIMR mabibo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa Kituo cha tiba asili cha NIMR mABIBO, Dkt. Nyigo Vitus akitoa maelezo wakati wa Ziara ya Baraza la NIMR ya kukagua maendeleo ya ujenzi na Usimikaji wa Mitambo katika kiwanda cha dawa asili kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. Yunus Mgaya akizungumza wakati wa Ziara ya Baraza la NIMR ya kukagua maendeleo ya ujenzi na Usimikaji wa Mitambo katika kiwanda cha dawa asili kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Prof. Yunus Mgaya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Ziara ya Baraza la NIMR ya kukagua maendeleo ya ujenzi na Usimikaji wa Mitambo katika kiwanda cha dawa asili kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wa baraza la NIMR wakipata maelekezo ya dawa zilizozalishwa katika kiwanda cha Dawa asili wakati wa Ziara ya Baraza la NIMR ya kukagua maendeleo ya ujenzi na Usimikaji wa Mitambo katika kiwanda cha dawa asili kilichopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...