Na Jane Edward, Arusha
Serikali imesema inajiandaa kupokea ndege mpya ya mizigo 767 pamoja na ndege mpya mbili za masafa ya kati ikiwa ni pamoja na kuangalia ndege mpya zinazokuja sanjari na utoaji wa mafunzo kwa marubani na wahandisi pamoja na wasimamizi wa ndege.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege la Tanzania ATCL Ladislaus Matindi wakati alipotembelewa na timu ya viongozi wa juu wa kampuni ya utengenezaji wa ndege za Boeing katika uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.
Matindi amesema kuwa kwa sasa wamejiandaa vizuri kuhakikisha wataalamu wa ndege kwa maana ya wahandisi,marubani wote kutoka Tanzania na wamejiandaa vizuri kupokea ndege hizo.
Ameongeza kuwa katika mazungumzo na ugeni huo pia wamezungumzia changamoto pamoja na kuangalia ni namna gani wanaweza kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya shirika hilo.
"Kwa sasa hivi ndege yetu moja inafanyiwa marekebisho ikiwa ni kila baada ya miaka mitatu lazima ndege iangaliwe kwaajili marekebisho mbalimbali ili kuendelea kubaki katika ubora unaotakiwa"Alisema Matindi
Aidha Matindi amesema wanaishukuru Serikali ya Mama Samia kwa kuendelea kuwajengea uwezo shirika hilo ambapo kwa sasa hawaazimi vifaa kutoka nje,vifaa vyote vinatoka Air Tanzania,mafundi na wanapunguza gharama tofauti na ilivyokuwa hapo awali .
"Uwekezaji uliofanywa na watanzania katika ndege hizi ni mkubwa na tuna ahidi kuendelea kukuza shirika hili na kuwafanya watanzania kupita kifua mbele wakifurahia shirika lao popote waendapo"Alisema
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Hai kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Juma Irando amesema anawahakikishia Watanzania kuwa Tanzania iko salama na hayo ni matunda ya Rais Samia kwa kuiwezesha ATCL kuwa na karakana yao wenyewe.
Modesta Mwanjala ni kiongozi wa uhandisi kutoka Air Tanzania anasema kuwa ndege hizo zipo salama na wanafata sheria kwa mujibu ya miongozo iliyowekwa huku akiwatoa hofu Watanzania kuwa na Imani na Wataalamu wazawa.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege Tanzania ATCL Ladislaus Matindi mwenye suti ya blue akipanda kwenye ndege kwaajili ya kujionea matengenezo yanayoendelea.
Wakiwa kwenye matembezi kujionea shughuli zinazoendelea katika karakana ya shirika hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...