Adeladius Makwega–MAKOLE

Oktoba 5, 2022 nikiwa Mji wa Serikali Jijini Dodoma, nilipata bahati ya kumuona Ali Mayai Tembele akipita katika ofisi moja ya watumishi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo alimsabai mwanakwetu. Katika msafara wake ndugu Tembele ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini aliambatana na Ado Komba ambaye mimi natambua cheo chake cha awali ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo nchini kabla ya kuondolewa mwalimu Yusuf Singo.

Mwalimu Ado Komba ni kiongozi ninayeheshimiana naye sana na kumfahamu muda mrefu tangu akiwa TAMISEMI, siku hiyo alimuongoza ndugu Tembele nilipo na kusema neno hili,

“Huyu jamaa unayemuona anaitwa Kazimbaya Makwega, hatari sana, kuwa naye makini.” Aliyasema maneno haya kwa utani huku na mwanakwetu akicheka, akilini mwangu nikatafakari sana kwa kuwa Ado Komba ni mwalimu wa michezo wa muda mrefu na utani katika michezo una nafasi kubwa katika kupeleka ujumbe. Nilijiuliza kwanini Mwalimu Komba anitanie mbele ya kiongozi mgeni? Kwani asinitanie hivyo tukiwa wenyewe ? Mbona hajawai kunitania hivyo? Nikatafakari hilo nikasema hapa na mimi niseme jambo kwa kiongozi huyu mpya wa michezo nchini Tanzania ambaye ndiyo kwanza ameingia ofisini. Ofisi nilipokuwapo kwa juu kulikuwa na picha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ikishuhudia Tembele na Komba nikizungumza nao.

“Tembele wasaidie hawa jamaa, kwa sasa ni sawa na ile simulizi ya nitampiga mchungaji wa kondoo na kundi lake litatawanyika, waweke pamoja, fanya nao kazi kwa karibu hili tupate maendeleo ya michezo nchini Tnazania.”

Ali Mayai akacheka, wakaondoka zao kuelekea ofisi zingine za wizara hiii.

Kwa bahati nzuri Mkurugenzi wa Michezo aliyeondoka ndugu Yusuf Singo binafsi ninamfahamu na nimewahi kuingia nae katika vikao kadhaa vya kamati za Bunge akiwa na viongozi kadhaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na baadaye Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Ninaweza kusema haya dhidi yake,

“Yusufu Singo alikuwa ni Mkurugenzi mwenye umahiri mkubwa katika propaganda ya michezo na hata anapolielezea suala la michezo kwa mtu anayefahamu elimu hii na hata yule ambaye hafahamu elimu hiyo ilikuwa ni rahisi mno kumuelewa, kwa hakika alikuwa anafahamu michezo ya darasani vizuri sana. Lakini Singo hakuwa mchezaji wa moja kwa moja kitu ambacho Ali Mayai Tembele anacho japokuwa Tembele nayeye kuwa mahiri katika propanganda ya michezo yote anakosa, lakini mchezo wa soka propaganda yake anaifahamu.”

Tembele kuwa mchezaji wa mchezo mmoja shida yake bado anahitaji mno elimu ya kuwekeza kujifunza uongozi katika michezo mingine kama vile riadha, ngumu, netibali na kadhalika na kuifahamu hiyo ndiyo kurugenzi ya michezo, ili afuzu katika hilo ndugu huyu anawajibu wa kuwakusanya kondoo waliotayawanyika baada ya kupigwa mchungaji wao.

Ninaamini Ili kuboresha michezo nchini nafasi kama hizi wakati mwingine kama itatupendeza tuchukue maafisa michezo waliopo katika katika vyombo vya ulinzi ili waje kujenga ari ya michezo kitaifa na mwisho mafanikio ya michezo.

Swali ambalo linabaki kwa kila mmoja wetu kama Yusuf Singo alishindwa je alishindwa yeye mwenyewe peke yake? Sie tulio chini au wale walio juu hawakumkwamisha? Je adhabu inapaswa kuendelea kwa walio chini na walio juu yake? Je Tembele hayawezi kumkuta yalimkuta Yusuf Singo?

“Katika michezo tukishinda tunashinda sote; tukifungwa tunafungwa sote.” Hii tafakari sana msomaji wangu.

Mwanakwetu ninaomba niishie hapo kwa leo,  kwaheri Yusuf Singo Karibu Ali Mayai.

makwadeladius@gmail.com

0717649257Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...