NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MBEYA
WALIMU
nchini wamehimizwa kuweka amana zao kwenye benki ya Mwalimu Commercial Bank
Plc. Ili waweze kupata manufaa zaidi.
Hayo
yamesemwa na Kaimu rais wa Chama cha Walimu nchini, Mwalimu Dinna Mathamani
kwenye Mkutano Mkuu wa sita wa Wanahisa wa benki hiyo uliofanyika jijini Mbeya
Alhamisi Oktoba 6, 2022.
“kwa
sisi wana hisa tunaona mwelekeo mzuri wa benki yetu, mimi kama kiongozi wa
Chama cha Walimu nawahimiza walimu kuendelea kuweka amana zao kwenye benki
yetu ili tuendelee kupata manufaa zaidi.” Alisema.
Kwa
upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa CWT, Mwalimu Maganga Japhet alisema wao kama
chama wamekuwa bega kwa bega na benki na kwa sasa watumishi wote wa chama
wanapitishia mishahara yao kwenye benki ya Mwalimu Commercial Bank.
“Walimu
wana hisa asilimia 35.29% hivyo ni wajibu wetu
kuhakikisha tunaiimarisha benki yetu na ili kufikia malengo ya kuanzishwa
kwake.” Alifafanua Mwalimu Japhet.
Awali
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mwalimu Commercial Bank Plc. Francis Cecil
Ramadhani amewapongeza wanahisa wote kwa hatua ambayo benki imefikia kwa sasa,
kwani kuanzia Julai mwaka jana benki imeanza kutengeneza faida mwezi hadi
mwezi.
“Benki pia imeweza kukuza thamani ya mali zake kwa asilimia 53% na kufikia shilingi za Kitanzania Bilioni 58 kutoka shilingi Bilioni 38.” Alifafanua Ramadhani.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc. Richard Makungwa, amewahakikishia wanahisa na wateja wa benki hiyo kuwa benki imeendelea kuimarisha mifumo ya kidijitali (TEHAMA), ambapo mteja anaweza kupata huduma za kibenki akiwa mahala popote kwa kutumia simu ya kiganjani *150*31# au MwalimuBank App, Mwalimu VISA card au MwalimuWaka.
“Nipende
kusema walimu ni mojawapo ya kundi la wateja wazuri sana najua wenzetu
wanawawinda, sisi pamoja na udogo wetu tunaweza kushindana na wenzetu walio
katika soko, nitumie fursa hii kuwahimiza walimu karibuni, rudini nyumbani,
nyumbani kumenoga ili muone faida na maana ya ninyi kunzisha chombo chenu cha
kifedha ambacho nia ilikuwa ni kuwakwamua kiuchumi.” Alihimiza Makungwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...