Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Lukiza Autism na muandaaji wa mbio ya Run 4 Autism Tanzania inayojihusisha na kutetea watu wenye hali ya Usonji/Autism, Hilda Nkabe amewataka wazazi wenye watoto wenye Usonji kutokata tamaa na kuwalea watoto wao kwa upendo, pamoja na changamoto zote wanazozipitia katika ulezi.
Akizungumza katika Kongamano la kwanza la Kitaifa la afya ya akili nchini lililofanyika katika ukumbi wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere ( JINCC ), jijini Dar es salaam. Mkurugenzi huyo ameiomba Wizara ya afya kutatua changamoto zinazowakabili wazazi wa watoto hawa, kama vile gharama kubwa za mazoezi tiba, uchache wa wataalam wa utambuzi wa hali ya Usonji na wataalam wa mazoezi tiba, uchache wa vituo vya afya vinavyotoa huduma za mazoezi tiba na shule au vituo jumuishi au maalum.
"Tatizo la usonji linawapata watoto wadogo ambapo dalili huanza kuonekana katika umri wa chini ya miaka mitano. Dalili zake kubwa ni changamoto za mawasiliano, changamoto katika kutengeneza mahusiano na jamii inayomzunguka, changamoto za kitabia na hisia.
Akipokea tuzo ya ubalozi wa afya ya akili kutoka kwa Waziri wa afya, Mhe Ummy Mwalimu, kutokana na mchango wake katika kuelimisha jamii juu ya afya ya akili hususan Usonji, bi Hilda Nkabe alimshukuru Mhe. Ummy mwalimu na Wizara ya afya kwa ujumla kutambua mchango wake kwenye sekta hii na kwa kufanikisha uwepo wa Kongamano hili la kwanza la kitaifa la afya ya akili na kufungua mazungumzo mapana ya Kitaifa kuhusu afya ya akili nchini Tanzania.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya isiyo ya kiserikali ya Lukiza Autism Foundation na muandaaji wa mbio ya Run 4 Autism Tanzania inayojihusisha na kutetea watu wenye hali ya Usonji/Autism, Hilda Nkabe akizungumza katika Kongamano la kwanza la Kitaifa la afya ya akili nchini lililofanyika katika ukumbi wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere ( JINCC), jijini Dar es salaa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...