Na Pamela Mollel,Arusha

Mbio maarufu nchini Serengeti Safari Marathon kufanyika November 12 mwaka huu katika hifadhi ya Serengeti upande wa Ndabaka gate

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha mratibu wa mbio hizo John Temu alisema mbio hizo hufanyika mara moja kwa mwaka katika hifadhi ya Serengeti

"Maandalizi ya tukio hili yamekamilika kwa asilimia kkubwa na tumeweza kuboresha T-shirt,Medali,Kofia na mambo mengine ya msingi"alisema Temu

Alisema watu watakao shiriki katika mbio hizo watapata fursa ya kufanya utalii wa ndani kwa kujionea wanyama katika hifadhi ya Serengeti

Aidha alisema lengo hasa la kufanya Marathon hiyo ni kuhamasisha utalii na michezo hapa nchini jambo ambalo litawapa watu fursa ya kupenda utalii na michezo

Aliongeza kuwa mbio hizo zina kilometa 42,kilometa 21,kilometa 10 na kilometa 5

Pia aliongeza kuwa katika kuweka sawa wakimbiaji wamepata bahati ya kumleta kocha wa marekani ambaye kazi yake kubwa ni kuwapa mafunzo kabambe wachezaji wa mbio za ndani na zakimataifa

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha riadha mkoa wa Arusha Gerard Babu alipongeza waandaaji wa mbio hizo kwa kuwatambua wanariadha chipukizi

Alisema kuwa ujio wa kocha kutoka marekani umekuwa neema kwa wanariadha nchini ambapo kocha huyo aliweza kugawa vifaa kwaajili ya wanariadha

Diamia Christian na wakimbiaji wengine walimpongeza kocha huyo kwa kugawa viatu na Tshirt kwaajili ya kuhamasisha riadha nchini

Marathon ya serengeti safari ilianza mwaka 2018 ikiwa na wakimbiaji 400, kila mwaka ilikuwa ikiongeza idadi ya wakimbiaji ambao 2021 wakimbiaji 1500.

Mratibu wa mbio za serengeti safari Marathon John Temu akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya mbio hizo kufanyika November 12 mwaka huu katika hifadhi ya Serengeti

Kocha kutoka Marekani Alexander Crowther akizungumza na waandishi
Damian Christian mwanariadha

 Mwenyekiti wa chama cha Riadha mkoa wa Arusha Gerard Babu akizungumza na waandishi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...