Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chemba ya Biashara ya Tanzania, Zanzibar na Chemba ya Biashara ya Qatar.

Kwa upande wa Chemba ya Biashara ya Tanzania, mkataba ulisainiwa na Rais wa Chemba hiyo Paul Koyi, huku pia ukisainiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC) Ali Suleiman Amour.

Aidha, kwa upande wa Qatar mkataba huo umesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya nchi hiyo Muhammed bin Ahmed Al Kuwari uliofanyika Jijini Doha.

Lengo la Mkataba huo ni kuimarisha Biashara na Uwekezaji kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Qatar hususan kwenye sekta za utalii, miundombinu, ujenzi wa mahoteli na usambazaji wa gesi.

Mbali na utiaji saini huo, Rais Samia amefanya mazungumzo na Waziri wa Fedha wa Qatar, Mhe. Ali bin Ahmed Al-Kuwari ambapo wamejadili masuala ya kikodi baina ya nchi hizo mbili, uwekezaji, biashara, gesi, ufugaji, utalii na kilimo.

Vilevile, katika mazungumzo ya Rais Samia na Waziri wa Afya wa Qatar, Mhe. Dkt. Hanan Mohamed Al Kuwari wamekubaliana wataalamu wa Tanzania wabadilishane uzoefu kwenye sekta ya afya hasa katika huduma za kibingwa na za dharura.

Rais Samia pia katika ziara yake ya kikazi alifanya mazungumzo na Amiri wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al Thani, wafanyabiashara wakubwa na kuhudhuria Mkutano wa Ubunifu wa Afya Duniani (World Innovation Summit for Health) uliomalizika leo katika Kituo cha Elimu cha Multaqa Jijini Doha.

ZuhuraYunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chemba ya Biashara ya Tanzania (iliowakilishwa na Rais wake Paul Koyi), Zanzibar (iliyowakilishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC) Ali Suleiman Amour pamoja na Chemba ya Biashara ya Qatar iliyowakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Qatar Muhammed bin Ahmed Al Kuwari. Hafla ya utiaji saini wa Mkataba huo umefanyika Doha nchini Qatar 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Qatar Muhammed bin Ahmed Al Kuwari pamoja na ujumbe wake, Doha nchini humo tarehe 06 Oktoba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Qatar Muhammed bin Ahmed Al Kuwari mara baada ya mazungumzo, Doha nchini Qatar tarehe 06 Oktoba, 2022. Kushoto ni Rais wa Chemba ya Biashara ya Tanzania (TCCIA) Paul Koyi na kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC) Ali Suleiman Amour


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Qatar Muhammed bin Ahmed Al Kuwari mara baada ya mazungumzo, Doha nchini Qatar tarehe 06 Oktoba, 2022. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...