Mmoja wa wanafunzi walioshiriki katika programu ya kompyuta akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Mkurugenzi wa kanda-VETA Kanda ya Dar es salaam, Habibu Bukko baada ya kuibuka washindi katika maonyesho ya Vijana wa Sekondari Kutoka wilaya ya Temeke

 



KATIKA kuongeza upeo wa Vijana kupitia miradi ya Kimaendeleo, Shirika lisilo la Kiserikali la BRAC Maendeleo Tanzania Mwezi Julai mwaka 2022 ilianzisha programu ya "coding bootcamp" ambapo wanafunzi wanaoshiriki program ya kompyuta walielekezwa kuwasilisha mawazo ya biashara ambayo yataangalia changamoto zilizopo katika mazingira wanayoishi na kuzitatua kwa kutumia teknolojia.

Wanafunzi wengi waliwasilisha mawazo yao na wanafunzi 45 kati ya 120 walisailiwa kwenye kambi ya mafunzo ya kodi yaani "coding bootcamp na mwezi Agosti mwaka huu BRAC kwa kushirikiana na VETA Pamoja na AMCET Hub waliweza kutoa mafunzo kwa wanafunzi hao.

Akizungumza katika maonyesho hayo katika shule ya sekondari karibuni, Temeke, Mkurugenzi wa kanda-VETA Kanda ya Dar es salaam, Habibu Bukko alisema VETA Kanda ya Dar es salaam imeshirikiana na BRAC Maendeleo Tanzania pamoja na AMCET Hub Kwenye kambi ya mafunzo ijulikanayo kama “CODING BOOTCAMP” kwa wanafunzi 45 ambapo leo hii tumeweza kuyaona matunda ya mafunzo haya.

“Mmejionea wenyewe jinsi vijana hawa wameweza kuonyesha uwezo wao mkubwa wa uvumbuzi pamoja na utatuzi wa matatizo yanayayowazunguka kwenye jamii.Nipende kutoa wito kwa BRAC Maendeleo Tanzania pamoja na wadau wa maendeleo na elimu walioko hapa waweze kuangalia namna ya kuyaendeleza mawazo haya ya vijana walioshiriki programu hii,"alisema Bukko.

Kwa upande wake, Muwakilishi kutoka BRAC Maendeleo Tanzania Shukuru Musabila ameishukuru Serikali kuu ya Tanzania chini ya uongozi wa Raisi Samia Suluhu Hassan, na hasa wanapenda kutambua kipekee ushirikiano wa viongozi wa wilaya ya Temeke na vitongoji vyake ambao wameshirikiana nao kwa watoto wadogo na uwezeshaji kwa vijana.

"Tunawashuru sana kwa ushirikiano wenu.Tukiwa tumetoka kuadhimisha siku ya Mtoto wa Kike Duniani (International Day of the Girl Child-IDGC) tarehe 11 Oktoba 2022 ni matumaini yetu kama shirika kuwa kupitia mradi huu, program hii imeinua uwezo wa wanafunzi-hususani mabinti wa kike kufikiri kwa kina, kuwajengea uwezo wa uvumbuzi na utatuzi wa matatizo kwa kushughulikia changamoto za kijamii na kiuchumi na kuzigeuza kuwa mawazo muhimu ya biashara kwa kutumia maarifa ya TEHAMA," alisema Musabila.

"Toka mwaka 2020, tumekuwa tunatekeleza mradi huu wa Skills for their Future ambako ulianza kama mradi wa majaribio katika shule ya Sekondari Temeke. Ilipofika mwaka 2021 tulipanua wigo kwa kuongeza shule za sekondari tatu katika wilaya ya Temeke; yani shule ya Wailesi sekondari, Miburani sekondari na hapa tulipo shule ya Karibuni sekondari ambako mradi ulizinduliwa rasmi mwaka huu mwezi wa tatu (3) ikiwa ni ndani ya mpango wetu wa Uwezeshaji Vijana (Youth Empowerment),"

Mussbila alisema, Mradi huu unafanyika chini ya ufadhili wa shirika la TheirWorld lenye makao makuu nchini Uingereza na Mpaka sasa BRAC Maendeleo Tanzania kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo, kupitia mradi wa Skills for Their Future wamefanikiwa Kuongeza ushiriki wa wasichana katika TEHAMA ili kuongeza fursa zaidi za ajira kwa wasichana katika sekta ya teknolojia.

Aliongeza kuwa,  mradi huo umeweza kufikia vijana 652 kati ya hao 500 ni wasichana na 100 wakiwa wavulana wenye umri wa miaka 14 - 24 katika shule 3 za sekondari wilayani temeke ambako mradi huu unatekelezwa, pia Katika kuhakikisha uendelevu wa mradi tumeweza kutoa mafunzo haya kwa walimu 60 katika shule 3 za sekondari (za ambazo ni Shule za Karibuni, Miburani na Wailes zilizopo wilaya ya Temeke Dar es Salaam) wa kutoa mafunzo bora ya kusoma na kuandika kwa njia ya kidijitali.

Aidha,BRAC wameweza Kuboresha ushirikiano wa umma na binafsi na wadau ili kutoa mazingira wezeshi kwa vijana hasa wasichana, kushiriki katika sekta ya teknolojia inayokua Kwa kasi nchini Tanzania.

Moja ya makundi ya wanafunzi wa sekondari wakielezea juu ya mradi wao kwa mgeni rasmi Mkurugenzi wa kanda-VETA Kanda ya Dar es salaam, Habibu Bukko  wakati wa maonesho ya Programu ya Kompyuta kutoka Shule za Sekondari Wilaya ya Temeke.
 

Picha ya pamoja, wanafunzi walioshiriki Katika  Cooding bootcamp wakiwa na uongozi wa wawakilishi kutoka BRAC, walimu wa shule hizo pamoja na mgeni rasmi.
Timu kutoka Shule ya Karibuni iliyoibuka washindi ikiwa katika picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...