Pichani juu Mchungaji Mwipile Ismail wa Usharika wa Segerea aliyemshikia nafasi Mchungaji wa Usharika wa Kinyerezi akipokea albam hizo na kuzibariki Oltesh  Metili ambaye yupo kwenye matibabu.
Lilian  akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani

Na Khadija Kalili . 
MUIMBAJI wa nyimbo za Injili Lilian Naman amezindu a albamu mbili kwa mpigo ambazo zimepokelewa madhabahuni jana Jumapili Novemba 20 katika Kanisa la KKKT huku majina ya albamu hizo ni 'Nishike Mkono' na 'Upo Uwezekano' madhabahu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Kati Ushirika wa Kinyerezi.

Albamu hizo zilipokelewa kwenye madhabahu ya Kanisa hilo na kupokelewa na Mchungaji wa Kinyerezi na Ismail Mwipile wa Segerea na kuziombea dua njema ili zifikishe ujumbe wa neno la Mungu kupitia nyimbo za muimbaji huyo.

Uzinduzi wa albamu hizo ulifanyika mara baada ya ibada ya kwanza Jumapili kanisani hapo na kuhudhuriwa na waumini wengi wa Kanisa hilo.

Akiziombea baraka albamu hizo Mchungaji Mwipile alisema Mungu azipokee kazi za mikono za kijana Lilian na ziwe njia ya mafanikio ya jamii.

Mchungaji Mwipile baada ya kuziombea baraka alizinadi kwenye madhabahu hiyo na zikauzwa ndani ya kanisa.

Lilian Naman amezitaja nyimbo zilizoko kwenye albamu ya 'Nishike Mkono' ni Asante Baba, Habadiliki, Nishike mkono, Mama Rita, Wanitosha na Yesu ndiye Bwana huku zilizoko kwenye albamu ya 'Upo Uwezekano' ni Nikurudishie nini, Kwa Baba, Upo uwezekano, Hatuna mji, Udumuo, Tanzania Naipenda na Yesu ndiye Bwana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...