Tanzania inaendelea kuongeza juhudi za kuboresha
mazingira ya biashara nchini ili kuvutia wawekezaji zaidi wa ndani na nje. Kufuatia maendeleo
ya hivi karibuni ambayo ni pamoja na kuletwa kwa Sheria ya Uwekezaji Tanzania ya mwaka
2022, jukwaa la CEO Roundtable Tanzania (CEOrt) litafanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe  kuhusu nafasi ya Sekta Binafsi katika 
kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini kupitia uwekezaji.

Ikiwa na wingi wa fursa kwenye soko, Tanzania inatoa mazingira rafiki kwa wawekezaji. Kupitia
vipengele mbalimbali vilivyoboreshwa kwenye sheria mpya ya uwekezaji, Serikali inaendeleza
jitihada za kuvutia zaidi wawekezaji, na hivyo kuongeza ajira, kujenga viwanda na kukidhi
mahitaji ya ukuaji wa uchumi.
Kama sehemu ya malengo yake, jukwaa la CEOrt limedhamiria kuwezesha mijadala kati yasekta ya umma na sekta binafsi yanayolenga kuchunguza mabadiliko ya sera ili kujengamazingira rafiki ya biashara kwa maendeleo endelevu ya Tanzania. Sekta Binafsi ni sehemumuhimu ya kuchochea uwekezaji kutoka nje, na kama wawakilishi wa sekta hiyo, viongozi wabiashara ambao ni wanachama wa CEOrt watapata fursa ya kuendesha mazungumzo na Sektaya Umma kuhusu masuala muhimu ndani ya uwekezaji. 

CEOrt inatazamia kupata maoni ya sekta zote mbili kuhusu kuboresha uwekezaji nchini, na
kutazama jukumu la Sekta Binafsi katika kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini
kupitia kuwekeza.


 Kiongozi mkuu wa 
CEO Roundtable - Tanzania  David Tarimo Akizungumza na vyombo vya Habari

 

Kuhusu CEO Roundtable - Tanzania

Shirika linawakilisha Wakurugenzi Wakuu kutoka kampuni karibia 200 zinazoongoza nchini
Tanzania kutoka sekta mbalimbali za uchumi kwa madhumuni ya pamoja ya kuongeza matokeo
katika uongozi na ustawi endelevu wa jamii na uchumi wa nchi. Kwa pamoja, wanachama wa
CEOrt huchangia katika uchumi wa Tanzania kupitia ukusanyaji wa kodi, ajira, kujenga uwezo,
kuhamisha teknolojia na kuongeza ujuzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...