BENKI
ya Biashara ya DCB imesema ushindi wa benki bora katika utoaji huduma
kwa benki zenye ukubwa wa kati ilioupata, umetokana na mabadiliko
makubwa iliyoyafanya katika mfumo mzima wa utoaji wa huduma kwa wateja
wao.
Akizungumza katika hafla za utoaji zawadi za Tuzo za Chaguo
la Mlaji Afrika (CCAA) jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa
DCB, Godfrey Ndalahwa alisema ushindi huo uliotokana na uboreshaji
mkubwa walioufanya katika huduma zao umekuja kwa wakati mzuri kipindi
hiki DCB ikisherehekea miaka 20 tokea ilipoanzishwa.
“Kwa niaba
ya familia ya DCB, napenda kushukuru sana wateja wetu na wasio wateja
wetu kwa kutupigia kura kwa kuwa benki bora kabisa nchini kwa kutoa
huduma bora, kupata tuzo hii kunazidisha furaha yetu wakati tukiendelea
kusherehekea miaka 20 ya benki yetu.
“Mimi na wafanyakazi
wenzangu tunafuraha kuona wateja wetu wameweza kuona uboreshaji mkubwa
tulioufanya wa jinsi tunavyowahudumia, hii ni safari tuliyoanza miaka
minne iliyopita na tunashukuru kuona matunda yake yanaonekana na wateja
wameweza kuyaona,” alisema Bwana Ndalahwa.
Pamoja na hayo
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa mafanikio hayo wao kama wanafamilia wa
DCB wanayachukulia kama changamoto ya wao kuzidi kuboresha zaidi huduma
zao na kuwa zaidi ya mahali walipo.
Hii ni mara ya pili kwa DCB
kushinda tuzo hii japo kwa mara ya kwanza mwaka 2021 ilitwaa ushindi wa
pili wa tuzo hizi zenye lengo la kuleta ushindani kati ya makamapuni na
biashara mbali mbali barani Afrika, kuhamasisha utoaji huduma na bidhaa
bora kwa wateja pamoja na kutambua kazi bora za watoa huduma.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya DCB, Dk. Amina Baamary (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa (wa nne kushoto), pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, wakishangilia mara baada ya kupokea tuzo ya mshindi wa kwanza ya Benki Bora kwa kutoa Huduma Bora kwa Wateja nchini kwa mwaka 2022 katika hafla ya utoaji zawadi kwa washindi wa Tuzo za Chaguo la Mlaji Afrika (CCAA) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...