Kampuni ya Gf Terucks & Equipment Ltd inajivunia mafanikio iliyoyapata kwa kipindi cha miaka 15 katika sekta ya uuzaji wa magari ya Mizigo na Mitambo nchinI
Hayo yamesemwa wakati wa uzinduzi wa chama cha wamiliki wa Magari ya mizigo na mitambo nchini katika hafla iliyofanyika jijini Dar es saaam
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa kitengo cha Biashara na masoko wa kampuni ya Gf Trucks & Equipment’s Ltd ,Salman Karmal alisema kutokana na sheria za uwekezaji nchini kuwa rafiki wao kwa kipindi cha miaka 15 wameweza kufungua kiwanda cha kuunganisha magari , GF Vehicle Assemblers kilichpo Kibaha mkoani Pwani
Pia lisema wa kwa kuunda chombo cha pamoja ni hatua moja wapo katika sekta ya usafirishaji kwani kupitia umoja huo tyr itakuwa rahisi chamngamoto zao kutatuliwa kwani hapo awali walikua hawana jukwaa la pamoja na kuwasemea tofauti na tasnia zingine na wao GF kama walezi wa umoja huo watakua bega kwa beka kuhakikisha unakuwa na tija kwa taifa kwa ujumla.
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Wamiliki wa Matipa Tanzania (TTMOA), Emmanuel Moshi aliiiomba Serikali ili kuwanufaisha wakandarasi wazawa kwenye miradi inayoendelea nchini, kabla ya mipango ya utekelezaji waitwe watoe maoni yao.
Alisema kupitia TTMOA wanauwezo wa kutekeleza miradi mikubwa ya Serikali na hakuna haja kuyatumia makampuni ya nje kutekeleza miradi hiyo.
"Tunaiomba Serikali iangalie umuhimu wa mitambo hii inayoingizwa nchini,tunalipa kiwango kikubwa cha kodi,"alisema. Chama Cha Wamiliki wa Mitambo Tanzania kilianzishwa mwaka 2018 na mpaka sasa kina wanachama 150
Kwa upande wa serikali Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete aliwata wakandarasi wote nchini kuhakikisha wanaimarisha Umoja wao kupitia chama hicho.
"Ili mambo yaende vizuri ni lazima muwe katika Umoja, kupitia chama hiki Serikali itaendelea kuwasiliza, wakandarasi wote wenye magari, wasio na mitambo hata wale wasio wakandarasi na wanamiliki mitambo wajiunge na chama hiki penye umoja kuna maendeleo,"alisema.
Mwakibete alisema ili taifa liendelee linahitaji ujenzi hivyo TTMOA ni nguzo muhimu kwani imechagua upande ambao Serikali inaweka nguvu.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe.Atupele Mwakibete akizungusha kifaa maalumu kuashiria uzinduzi wa Chama cha Magari ya mizigo na mitambo nchini (TTMA) jijini Dar es salam .Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd, Ally Jawad Karmal kushoto ni Salman Karmal mkuu wa kitengo cha Biashara na masoko wa GF na Kulia ni Mwenyekiti wa Chama (TTMA) Emmanuel Moshi
Wadhamini waku wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa huku wakiwa na zawadi walizokabidhiwa na kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...