Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Kamati ya kuthamini Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo yanatolewa na LST imetoa rai kwa Wizara ya Katiba na Sheria na Mahakama ya Tanzania kuitafutia sehemu nyingine Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ili kuanzishwa kwa Mahakama ya Wilaya itakayotumika kikamilifu kutoa mafunzo hayo ya Uanasheria kwa vitendo LST.
Hatua hiyo imekuja baada ya Kamati hiyo kubaini kuwa Mahakama iliyojengwa katika Taasisi hiyo ya LST kama sehemu ya miundombinu ya kuendeshea mafunzo kwa vitendo, kuendelea kutumiwa na Mahakama Kuu Divisheni hiyo ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kuendeshea mashauri mbalimbali.
Akisoma taarifa mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya kutathmini Mafunzo, LST, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema moja ya sababu waliyobaini ni kuwa Taasisi ya LST kutokuwa na Mahakama ya kufundishia mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo.
“Kamati imebaini kutokuwepo Mahakama ya kufundishia kwa vitendo ili kuwawezesha Wanafunzi kujifunza kwa kushuhudia wenyewe mashauri yanavyoendeshwa Mahakamani, nyaraka zinazotegemewa na weledi katika kujenga hoja na utetezi”, amesema Dkt. Mwakyembe.
Dkt. Mwakyembe amesema: “Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa haina mchango wowote katika mafunzo ya Uanasheria kwa vitendo kutokana na unyeti wa mashauri yanayoendeshwa hapo ambayo kiusalama hayaruhusiwi watu wengi pamoja na Wanafunzi kusogelea karibu.”
Hata hivyo, awali Mahakama hiyo iliamuliwa kuanza kazi ndani ya eneo la Taasisi ya LST kwa muda na baadaye iipishe Mahakama ya Wilaya ambayo itatumika kikamilifu katika kuendesha mafunzo kwa vitendo na kuruhusu mfumo wa Kielektroniki unaounganisha Mahakama na Darasa kuanza kufanya kazi na kuwezesha Wanafunzi kushuhudia mienendo ya mashauri wakiwa madarasani.
Kamati hiyo iliundwa Oktoba 13, 2022 na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro ili kutathimini Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) baada ya mjadala mkubwa nchini kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya Mitihani ya ‘Law School’ ya Kundi la 33 mwaka wa masomo 2021-2022.
Home
HABARI
MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA RUSHWA KUTAFUTIWA SEHEMU NYINGINE KUPISHA MAFUNZO KWA VITENDO LST
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...