MBUNGE Viti Maalum Nusrat Hanje, ambaye ni mleta maombi namba 15 katika kesi iliyofunguliwa na wabunge 19 wa viti maalumu (Chadema) wakipinga kufukuzwa ndani ya chama hicho, amedai kuwa vyama vya siasa vinauwa ndoto za vijana wengi.
Amedai anashangaa chama Chake (Chadema) kinakana hakijamdhamini ili tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC), imteue kuwa mbunge viti maalumu wakati kilimuahidi kuwa atakuwa Mbunge wa viti maalumu.
Mapema wakili Kibatala alimhoji Nusrat kwamba, Chadema kupitia kiapo chake kinzani katika kesi hiyo, kinasema hakijamdhamini kuwa mbunge viti maalum.
Nusrat amedai hayo leo Novemba 4,2022 mbele ya Jaji Cyprian Mkeha wa Mahakama Kuu Masijala Kuu wakati alipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kuhojiwa na wakili wa wajibu maombi Peter Kibatala.
Amedai kuwa, hata alipokuwa gerezani akikabiliwa na shauri la jinai, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika walishiriki mchakato wa kumtoa ndani.
"Amedai katika Chama alikuwa akipewa ahadi za kuwa Mbunge na alikuwa kiongozi mwandamizi...." Mwenyekiti na Katibu Mkuu walikuja gerezani nimesaini wakasema you don't have to worry. Kuna vitu vingine tunashangaa vinakuja, nimekuwa- sponsored Kwa mujibu wa mchakato na wanaofanya uteuzi ni tume," amedai Nusrat.
Akijibu swali la Kibatala kuwa kwa nini katika madai yake hakuona ni suala la msingi kuiomba mahakama kuamua madai ya chama hicho kwamba hakijawahi kumteua kuwa Mbunge wa viti maalum sababu alikuwa gerezani?
Nusrat akadai kuna mambo mengi ya kuyaongelea "ndiyo maana nimekuja kwenye mahakama hii sababu there is a lot ya kusema. Mimi sio mwendawazimu tunajidhalilisha ndiyo maana nimeomba turudi kwenye Chama kuzungumza."
Nae wakili Hekima Mwasipu alimuuliza Nusrat kama anaifahamu fomu namba nane inayotolewa na NEC Kwa ajili ya uteuzi wa wabunge viti maalumu Nusrat akajibu kuwa anaifaham.
Wakili Mwasipu: je unafahamu kuwa chama kikishamteua mtu kuwa mbunge au jina lake likishaenda NEC, lazima ajaze fomu hiyo
Nusrat: ndio nafahamu
Wakili : he ulijaza fomu hiyo,?
Nusrat: ndio nilijaza
Wakili: ulijazia wapi na nani alikupa fomu hiyo uijaze wakati ulikuwa gerezani hadi usiku wa Novemba 23,2020 ulipoachiwa na kesho yake Novemba 24,2020 ukaenda kuapishwa bungeni Dodoma?
Nusrat: nililetewa gerezani na Mnyika kati ya mwezi Julai na Novemba 2020.
"Kwanza itambulike kwamba fomu zinazohusiana na masuala ya uchaguzi nililetewa gerezani na katibu mkuu wa chama John Mnyika. Na haikuwa kitu cha kushangaza sababu nilikuwa katibu mkuu wa vijana hivyo nimekuwa nikisaini nyaraka....," Ameongeza Nusrat.
Pia amedai alikuwa anatembelewa na viongozi wa chama ambao ni Mwenyekiti na katibu akiwa gerezani na hata alivyotoka gerezani aliwapigia simu wakamuuliza kama yuko fit akawaambia yuko fit
"Nimepigiwa na viongozi wa chama akiwepo Mwenyekiti na katibu mkuu akaniambia tarehe 24 Novemba 2020 nikaapishwe na waliniambia watanitetea katika nafasi niliyogombea," amedai Nusrat.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...