Na Jane Edward, Arusha.

Uongozi wa mkoa wa Arusha umepokea miti ya matunda 30,000 kutoka Kanisa la Yesu kristo la watakatifu wa siku za mwisho kwa ajili ya kukabiliana na ukame mkoani Arusha.

Itakumbukwa kuwa katika siku za hivi karibuni hali ya ukame unaotakana na mabadiliko ya tabia nchi umezidi kukua kwa kasi huku jitihada mbalimbali zikifanyika kuondokana na hali ya ukame.

Akizungumza wakati wa kukabithi miche hiyo ya matunda ,Rais wa kanisa hilo,John Kasongo amesema kuwa, kanisa hilo limefikia hatua ya kutoa miche hiyo ya matunda kwa ajili ya kusaidia maswala ya usalama wa chakula kwa mkoa wa Arusha.

Amesema ,kanisa limekuwa likisaidia maswala mbalimbali ya kijamii katika mikoa mbalimbali ikiwemo elimu,afya na maswala ya usalama wa chakula .

Amebainisha kuwa,kwa upande wa maswala ya chakula wamekuwa wakitoa chakula endapo kunatokea majanga ya vita kwa ajili ya kusaidia wahanga kuweza kuondokana na changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Missaile Musa amesema kuwa wanashukuru kanisa kwa namna ambavyo wameona uhitaji uliopo wa miche ya matunda na kuweza kutoa kwa ajili ya kusaidia mkoa wa Arusha .

Amesema kuwa,miche hiyo ya matunda itasambazwa katika shule na taasisi mbalimbali za mkoa huo kwa ajili ya kutunza mazingira na kuweza kupata miti ya kivuli kukabiliana na ukame na kupata matunda pia,ambapo amesema bado wana uhitaji wa miche zaidi kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali.

Baadhi ya miche ya miti pichani.
Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Misaile Musa kulia akiwashukuru viongozi wa kanisa la watakatifu wa siku za mwisho mara baada ya kupokea miti hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...